Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema hayo katika mkutano wa hadhara mjini Istanbul kuelekea duru ya pili ya kura siku ya Jumapili kumchagua rais wa nchi hiyo | Picha: AA

Raia milioni 85 wa Uturuki watakuwa washindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Jumapili, aliapa Rais Recep Tayyip Erdogan katika mkesha wa uchaguzi huo.

"Wote ambao wana imani na utashi wa kitaifa, wana ndoto kwa nchi yetu na wanaona kuwa ni wa ardhi hizi watakuwa washindi katika uchaguzi wa Mei 28," Erdogan alisema katika mkutano wake wa mwisho mjini Istanbul Jumamosi kabla ya upigaji kura.

“Wale ambao licha ya chokochoko zote hizo, hawapendi kivuli kwenye uchaguzi, hawapuuzi utawala wa sheria au uhalali, na wanaoamini katika mabadiliko ya siasa za kiraia watahesabiwa kuwa washindi katika chaguzi hizi bila kujali matokeo,” aliongeza.

Uturuki unaelekea kwenye raundi ya pili ya kura siku ya Jumapili kumchagua rais baada wagombea kushindwa kufikia kiwango cha asilimia 50 katika duru ya kwanza wiki mbili zilizopita.

'Demokrasia itashinda'

Mnamo Mei 14 Muungano wa Watu wa Erdogan ulipata kura nyingi bungeni, huku kinyang'anyiro cha urais kikielekea kwenye duru ya pili kwani hakuna mgombea aliyepata kura nyingi au zaidi ya asilimia 50. Erdogan, hata hivyo, aliongoza kwa asilimia 49.52.

Katika duru ya pili, Erdogan atachuana na Kemal Kilicdaroglu, mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha Republican People's Party (CHP) na mgombea mwenza wa Muungano wa vyama sita vya upinzani Nation Alliance.

"Tutashinda kwa njia ambayo Uturuki yote pamoja na watu wake milioni 85 watashinda. Taifa letu lenye rangi zake zote litashinda, na demokrasia yetu, ambayo tulilipa bei kubwa itashinda," Erdogan alisema.

“Bila kujali chama gani cha siasa wanakipenda, wapiga kura wote wanaoonyesha mapenzi yao kwa njia halali watashinda,” aliongeza.

Erdogan alisema anaamini kuwa watu waliopigia kura vyama vya upinzani Mei 14 kama vile CHP, DEVA, HDP na IYI Party watahamia Muungano wa Watu siku ya Jumapili.

"Tutawaalika pia, ni watoto wa taifa hili. Natumai tutatembea pamoja," aliongeza.

TRT World