Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki mjini Ankara/ Picha: AA

Uturuki inafuatilia kwa "makini jaribio la mapinduzi lililofanywa na kundi ndani ya vikosi vya jeshi la Niger, ambalo lilisababisha kumuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum, ambaye alifika madarakani baada ya uchaguzi wa kidemokrasia, na kusimamisha shughuli zote za taasisi za kidemokrasia," ilisema taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.

"Tunatumai kuwa utaratibu wa katiba, amani ya kijamii, na utulivu wa Niger, nchi rafiki na ndugu, hautadorora" inaendelea taarifa hiyo.

Uturuki inahakikisha kwamba itaendelea "kuiunga mkono Niger wakati huu wa maamuzi muhimu."

TRT Afrika
Tovuti hii hutumia vidakuzi. Kwa kuendelea kuangalia tovuti hii, unakubaliana na utumizi wa vidakuziSera ya Vidakuzi
Kubali