Na
Edibe Beyza Caglar
Akiwa amevalia kilemba cha keffiyeh, mwezi Januari Steve Sosebee, alitunukiwa tuzo ya heshima na TRT kutokana na kazi za kibinadamu alizozifanya kwa miaka kumi huko Palestina.
“Msijisikie upweke,” aliwaambia Wapalestina wakati akipokea tuzo hiyo.
Sosebee amevuka vigingi mbalimbali kutokana na utayari wake, hususani kwa watoto wa Kipalestina wanaokabiliwa na ukandamizwaji kutoka Israeli.
Mwaka 1991, akiwa pamoja na marehemu mke wake Huda Al Masri, Sosebee alianzisha mfuko wa kuwasaidia watoto wa Kipalestina (PCRF) kwa nia ya kutoa huduma za afya na misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina.
Ilipofika mwaka 2024, Sosebee alianzisha taasisi ya HEAL Palestine, ambayo imejikita kwenye masuala ya Afya, Misaada na Uongozi na vile kuwasaidia wahitaji.
Sosebee aliweza kuwasaidia zaidi ya watoto 2,000 wa Kipalestina kupitia jitihada zake.
Yafuatayo ni mahojiano ya Sosebee kama alivyofanya na TRT World.
TRT World: Ulipata wapi wazo la kuanzisha taaisisi ya kuwasaidia watoto wa Kipalestina?
Steve Sosebee: Nilitembelea Palestina, kwa mara ya kwanza mwaka 1988, wakati wa vita vya kwanza vya Intifada. Kama tu ilivyo kwa wanafunzi wengine wa uandishi wa habari, tulitembelea eneo linalokaliwa la West Bank na Gaza, na tuliweza kujionea hali halisi ya maisha katika maeneo hayo. Safari ile ilibadilisha kabisa maisha yangu.
Hapo awali, nilikuwa na jukumu la kuwaelemisha Wamarekani kuhusu hali halisi ambayo ilikuwa haijulikani kwa wamarekani wengi kwa kipindi hicho. Sidhani kama Wamarekani walikuwa na uelewa wa ubaguzi wa namna ile.
Kila kitu kilibadilika baada ya kuwahudumia ndugu zetu waliojeruhiwa katika mlipuko uliotokea West Bank. Niliwaleta Ohio kwa matibabu.
Jumuiya ya Wapalestina, Waarabu, walijitolea kuwahudumia. Kulikuwa na hisia za huruma kwa watoto. Ndipo nilipogundua kuwa kazi za binadamu ni chanzo cha mabadiliko.
Simulizi za watoto hao zikaangaziwa na kwa mara ya kwanza, Wamarekani waliona watoto wa Kipalestina wakiwa na nyuso za furaha.
TRT World: Vyombo vya habari vya magharibi vinawatazamaje Wapalestina?
Sosebee: Uonevu wa Wapalestina ni wa makusudi kabisa. Watoto wa Gaza wanaonewa kwa kutoonekana kuwa ni binadamu huku vyombo vya habari vikiwa mstari wa mbele kutekeleza hilo.
Hata leo, bado kuna taariza za upendeleo. Taarifa hizo hizo huripotiwa tofauti ikiwa zinawahusisha Wapalestina au Waisraeli.
Vyombo vya habari, ikiwemo New York Times na CNN, vinaendelea kuchuja ukweli na badala yake kuongeza maoni yao: mauaji ya watoto hayaruhusiwi, lakini kila mara huwa yanahalalishwa kwenye vyombo vya habari vya Marekani.
Mitandao ya kijamii imebadilika, huku majukwaa kama vile TRT World, wanahabari wa kujitegemea wanawapa watu fursa ya kujionea ukweli halisi.
Hii ndio sababu ya kushambuliwa kwa waandishi wa habari wa Palestina. Watabakia kuwa mashujaa, wao pamoja na madaktari na wasaidizi wengine.
TRT World: Mtoto yupi aliyekuvutia wakati wa kufanya kazi naye?
Sosebee: Wako wengi, japo kuna mmoja ambaye namkumbuka. Ana miaka 11, mvulana kutoka Gaza. Shambulizi la helikopta mwaka 1991, lilimfanya apoteze mkono wake na miguu yake miwili. Niliratibu matibabu yake jijini Los Angeles, kabla hata ya kuanzishwa kwa PCRF. Alijifunza kutembea kwa kutumia miguu yake bandia, akaweza kwenda shule na kufanya vizuri katika masomo yake. Hata Rais Bill Clinton alimuandikia barua ya kumpongeza.
Miaka kadhaa baadaye, alirudi Gaza na kuanzisha familia yake. Alikuwa ni mwenye matumaini muda wote. Tuliendelea kuwasiliana kwa njia ya ujumbe mfupi. Nimekuwa na ukaribu wa aina hiyo na watoto wengi. Hata hivyo, hatujawasiliana kwa kipindi cha miezi sita sasa, wala kusikia kutoka kwake. Sina uhakika kama bado yuko hao. Hicho ndicho kinachoniumiza.
TRT World: Unajisikiaje baada ya kushuhudia madhila yote hayo?
Sosebee: Kwa kweli ni ngumbu kwani Gaza imekuwa sehemu ya maisha yangu toka mwaka 1988. Gaza ni eneo pekee kwangu, inaumiza sana kuona namna ilivyoharibiwa. Nimepoteza marafiki na watoto niliyokuwa nawahudumia. Lakini naendelea kwenda huko nikiamini kuwa tunaweza kubadilisha kitu na kuleta mabadiliko.
Hapa Marakeni, tunao watoto 30 waliojeruhiwa wanaopokea matibabu kutoka taasisi ya Heal Palestine. Tumefungua hospitali iliyohudumia maelfu ya watu wa Gaza ndani ya miezi 16. Tumefungua shule. Tumefungua mabwalo ya vyakula na kuwapa watu wengi chakula.
Inaumiza kuona yanayoendelea lakini nasukumwa na ari ya kuleta mabadiliko. Changamoto kubwa ni kutegemea hayo matumaini. Nimeshuhudia watoto wasio na mikono, wanaohitaji upasuaji na baadaye wakawa wakubwa wakiwa na familia zao. Hakika inafurahisha.
Kinachonipa nguvu ni kuona watoto hawa wakikuwa na kuanzisha familia zao.Niliumia sana nilipompoteza mke wangu wa kwanza Huda Al-Masri kwa ugonjwa kansa ya damu mwaka 2009. Nilibaki na mabinti wawili wa kuwalea na ndicho kilichonipa msukumo wa kuwasaidia watoto wa Palestina.
Baadhi ya watoto niliowasaidia miaka 10, kwa sasa wamekuwa watu wazima wakiendesha maisha yao.
TRT World: Ulipokea tuzo ya heshima kutoka TRT, na katika risala yako ulisema haufanyi hayo yote kwa ajili ya tuzo, ulimaanisha nini?
Sosebee: Nilijisikia heshima kutambuliwa namna ile, japo tuzo si kila kitu. Kuwasaidia wenye uhitaji, hasa wakati wa mauaji ya halaiki, ni jukumu la msingi la binadamu linalopaswa kufanywa kwa unyenyekevu, na si jambo unalofanya kwa ajili ya kutambuliwa.
Nilizaliwa huru. Sikuwahi kupigania haki yangu. Lakini uhuru huo unakuja na wajibu wa kusimama na wale ambao hawana. Hiyo inajumuisha Wapalestina, pamoja na jamii zilizotengwa katika nchi yangu, zinazojitahidi kupata usawa. Nasimama nao, na ng'ambo na wale wanaoguswa moja kwa moja na sera za serikali zao.
Hali ya Gaza inazua hisia kali—hasira, kukata tamaa, kufadhaika. Lakini hisia hizo hazitoshi. Wapalestina hawahitaji huruma yetu; wanahitaji hatua. Kubofya "like" kwenye mitandao ya kijamii haitoshi. Lazima tuelekeze hasira zetu katika kazi yenye maana. Ndio maana nilianzisha HEAL Palestine.
Ikiwa, baada ya kujitolea maisha yangu kwa sababu, kuna jambo moja ambalo nimejifunza, ni hili: tunaweza kufanya tofauti, ikiwa tunachagua.