Muharrem Ince | Picha: AA

Kabla ya Muharrem Ince kuanzisha chama chake cha kisiasa, mwanasiasa huyo wa Uturuki alikuwa na historia ndefu ya kuwakilisha chama kikuu cha upinzani nchini humo, Republican People's Party (CHP), hususani kama mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2018.

Katika nafasi yake kama mgombea urais, Ince alipata zaidi ya asilimia 30 ya kura zote na hivyo kushika nafasi ya pili nyuma ya Recep Tayyip Erdogan wa Chama cha Haki na Maendeleo (AK Party), aliyepata asilimia 53.

Lakini kupanda kwake juu katika uongozi wa CHP, na baadaye kuondoka kwake kutoka kwa chama hicho, kulianzia katika ngazi ya mtaa katika mkoa wa mji wake wa Yalova, ambapo alizaliwa katika kijiji cha Elmalik mnamo Mei 4, 1964.

Huko Yalova, Ince alichukua nyadhifa mbalimbali katika mashirika yasiyo ya kiserikali kabla ya kuamua kwamba anataka kuingia bungeni, akiwa na umri wa miaka 38. Alijiunga na CHP mwanzoni mwa miaka ya 1990 kama mbunge wa Yalova na alihudumu kwa mihula minne.

Pia katika ngazi ya shinani, aliwahi kuwa rais wa mkoa wa Yalova kupitia Chama cha Mawazo cha Ataturkist (ADD), taasisi ya kiraia ambayo inaunga mkono mawazo ya mwasisi wa Taifa la Uturuki, Mustafa Kemal Ataturk, na hata alikuwa Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu ya soka ya Yalovaspor.

Kampeni ya urais, nyufa ndani ya CHP

Kabla ya mzee huyo wa miaka 58 kuvutiwa na siasa, shauku yake ya dhati ilikuwa kufundisha. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Uludag (sasa Chuo Kikuu cha Balikesir), ambapo alichukua shahada yake katika Kitivo cha Elimu cha Necatibey. Baadaye alifanya kazi kama mwalimu wa fizikia na mkuu wa shule katika shule mbalimbali za sekondari na taasisi za kibinafsi za kufundisha.

Ince aligombea uongozi wa CHP na alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti chini ya mwenyekiti Kemal Kilicdaroglu, nafasi aliyohudumu kati ya Juni 2010 na Agosti 2014.

Ince, ambaye ameoa mke wake Ulku na ana mtoto wa kiume anayeitwa Salih Arda, alichaguliwa tena katika nafasi hiyo mwaka wa 2011 na 2013. Alijiuzulu Agosti 2014 na nafasi yake kuchukuliwa na Levent Gok.

Wakati wa uchaguzi wa ndani mwaka wa 2014, Ince pia alichukua jukumu kubwa katika kumuunga mkono Vefa Salman, mgombea wa CHP katika nafasi ya Umeya wa Yalova. Na alibeba jukumu zito katika kampeni na wakati wa kuhesabu kura huko Yalova.

Lakini nyufa katika uhusiano wa Ince na CHP zilianza kuonekana kufuatia kushindwa kwa chama hicho katika uchaguzi wa urais wa 2014.

Ince alianza kumkosoa vikali kiongozi wa sasa wa chama hicho, Kilicdaroglu, baada ya mgombea mwenza wa urais wa CHP na Nationalist Movement Party (MHP), Ekmeleddin Ihsanoglu, kushindwa na Erdogan. Ince mara baada ya kutangaza kugombea uenyekiti wa chama.

Katika mkutano na waandishi wa habari wa Agosti 14, Ince alisema kwamba hataruhusu tena CHP kupoteza sifa mbele ya umma wa Uturuki na kudai chama hicho kinaendeshwa na wasomi wachache wanaotoka familia maarufu.

Aligombea uongozi wa chama lakini alishindwa katika kongamano la 2014 kwa kura za wajumbe 415 pekee dhidi ya 740 za Kilicdaroglu. Mzunguko uchaguzi uliofuatia, Ince aligombea tena kama mwenyekiti wa CHP.

Wakati wa Kongamano la 36 la CHP Februari 2018, Ince wakati huu alipata kura 447 kutoka kwa wajumbe wa chama huku Kilicdaroglu akipata kura 790 na kutangazwa kuwa kiongozi wa chama kwa mara nyingine tena.

Lakini Ince alichaguliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi wa urais wa mwaka huo. Kilicdaroglu alitangaza kuunga mkono kwa Ince kupitia CHP , na kugombea kwake kulitangazwa muda mfupi baadaye.

Kampeni ya Ince ya mwaka 2018 ilianza kwa mkutano wa uchaguzi huko Yalova chini ya kauli mbiu ambayo inatafsiriwa kwa "Muharrem Ince, hakikisho la Uturuki". Lakini mwisho, Erdogan alimshinda Ince. Kiongozi aliye madarakani alipata asilimia 52.6 ya kura huku Ince akipata asilimia 30.64 ya kura.

Baada ya Kongamano la 37 la CHP, Ince alitangaza kuwa ataanzisha chama kipya cha kisiasa kiitwacho Memleket Party mnamo Septemba 2020.

Alitangaza kujiuzulu kutoka CHP mnamo Januari 2021 na alijiuzulu rasmi mwezi mmoja baadaye.

TRT Afrika