Uturuki na Umoja wa Ulaya zinategemeana, amesema msemaji wa Tume ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya nje na sera za usalama.
Katika mazungumzo yake na jopo la wanahabari kutoka Uturuki mjini Brussels siku ya Jumatatu, Peter Stano alisisitiza kuwa kanda hiyo inatambua umuhimu wa Uturuki.
"Tunategemeana na tutakuwa na nguvu tukiwa pamoja," Stano alisema.
Hata hivyo, alidai kuwa mtazamo wa umoja huo unachangiwa na kanuni na maadili na kwamba hakuwezi kuwa na maendeleo iwapo hakutakuwa na maridhiano baina ya wahusika.
Kuhusu usitishwaji wa mazungumzo ya Uturuki kujiunga na umoja huo, Stano "alisikitishwa na hali hiyo akisisitiza umuhimu wa Uturuki katika eneo hilo la muungano."
Alipoulizwa kwa nini Uturuki inachukuliwa kama tu nchi ya jirani, badala ya mwanachama mtarajiwa, alisema, "Sioni chochote kibaya kuiona Uturuki kama nchi jirani," akisema kuwa ni fahari sana kuwa jirani wa Uturuki."
Mazungumzo ya uanachama wa Ankara ndani ya Umoja wa Ulaya
Uturuki iliomba kujiunga na Umoja wa Ulaya toka mwaka 1987 na amebakia kuwa mtia nia hiyo tangu mwaka 1999.
Mazungumzo ya uanachama wa Ankara ndani ya Umoja wa Ulaya yalianza mwaka 2005, lakini yalikwama baada ya 2007 kutokana na tatizo la Kupro na upinzani wa nchi kadhaa zilizopinga uanachama kamili wa Uturuki.
Utawala wa Kigiriki wa Cyprus ulikubaliwa kwa EU mwaka 2004, mwaka huo huo Wacypriots wa Ugiriki walizuia mpango wa Umoja wa Mataifa wa kumaliza mzozo wa muda mrefu.
Upinzani toka kwa Ufaransa na masharti ya kisiasa yaliyowekwa na Ugiriki na utawala wa Cyprus ya Ugiriki bado ni vikwazo vikubwa katika mchakato wa Uturuki wa kujiunga na Umoja wa Ulaya.