Wake wa viongozi wa Kenya, Serbia, Albania, Kroatia na Makedonia Kaskazini ni miongoni mwa wageni walikuwepo kwenye hafla hiyo, ambayo pia ilihudhuriwa na majina mashuhuri ya ulimwengu wa mitindo wa Marekani.
Emine Erdogan aliwahutubia wake wa wakuu wa nchi nyengine na wageni mashuhuri wa kigeni waliohudhuria maonyesho hayo yaliyoshirikisha bidhaa za nguo zilizotengenezwa kwa mikono na kuzalishwa kupitia taasisi za Wizara ya Elimu ya Uturuki na kuandaliwa, kwenye jengo la Uturuki, New York.
Emine alisema kuwa lengo la maonyesho hayo lilikuwa "kuongeza hazina za kipekee za kitamaduni za Anatolia kwenye urithi wa ulimwengu wa binadamu" huku akiongeza kuwa ufumaji huo uliopatikana enzi za kale ulimwenguni, ulipatikana Anatolia na kuanza miaka elfu 9 iliyopita.
Emine Erdogan ameongeza kuwa mafundi wa nguo wa kituruki wamesajiliwa katika orodha ya hazina hai za wanadamu ndani ya mfumo wa mkataba wa UNESCO wa Ulinzi wa Urithi wa Utamaduni Usioonekana.
Sifa kwa sekta ya nguo ya kituruki kutoka kwa wake wa wakuu wa nchi
Akizungumzia ufanisi wa sekta ya nguo ya Uturuki, Emine Erdogan alisema, " Sekta yetu ya nguo tayari ni mshirika muhimu katika soko za ulimwenguni tunavyozungumza. Tunakusudia kuimarisha sekta yetu ya nguo hata zaidi na ushonaji wetu wa jadi ambao tunatoa kwa masoko ya ulimwengu katika karne ya kituruki,"alisema.
Wake wa viongozi, walioonekana kuvutiwa na bidhaa zilizoonyeshwa, walisifu sekta ya nguo ya Uturuki na kumshukuru Emine Erdogan kwa mchango wake katika mradi wa ushonaji wa 'Atlas ya Uturuki'.
Programu hiyo pia ilihudhuriwa na mawaziri wa Uturuki wakiwemo Waziri wa Huduma za Familia na Jamii Mahinur Özdemir Göktaş, Waziri wa Viwanda na Teknolojia Fatih Kacır na Waziri wa Biashara Ömer Bolat.