Mama wa taifa wa Uturuki Emine Erdogan ameelezea Utayari wa Uturuki kuwapokea watoto yatima wa Gaza hadi kusitishwa kwa mapigano kwa kudumu kupatikana na hali ya kawaida inashinda katika eneo lililozuiwa.
Emine Erdogan aliambatana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwenye ziara yake rasmi ya Cairo, ambapo pia alikutana na mwenyeji wake wa Misri, Entissar Amer, baada ya karamu rasmi ya mapokezi Jumatano.
Wakati wa mkutano, suala la kuiongezea Gaza misaada na hali mbaya ya kibinadamu vilijadiliwa .
Suala la kuwalea na kuwalinda watoto walioachwa yatima na janga jilo la kibinadamu la huko Gaza, ambapo mashambulizi ya Israeli yameua zaidi ya Wapalestina 28,000, pia lilitiliwa mkazo.
Wito wa mshikamano kwa Gaza
Mama Emine Erdogan pia alitembelea Shirika la Mwezi Mwekundu la nchini Misri kukagua jitihada za shirika hilo katika kuisadia Gaza na vile vile wakfu wa Haya Karima ambapo, alisema, "ilikuwa shirika la kwanza kuwapo na timu kubwa ya wajitolea katika kuvuka mpaka wa Rafah."
Emine Erdogan alisisitiza hitaji la mataifa yote kuunganisha juhudi zao kwa Gaza.
Entissar Amer alielezea kuwa ziara hiyo ilileta furaha kubwa kwa watu wa Misri na kumpongeza kwa kuandaa Mkutano wa 'One Heart Summit' Novemba iliyopita mjini Istanbul.
Zaidi ya Wapalestina 28,000 wamepoteza uhai wao na kusababisha uharibifu mkubwa na uhaba wa mahitaji, tangu kutokea kwa uvamizi wa mpakani uliofanywa na kikundi cha Palestina cha Hamas mnamo Oktoba 7, na kuua watu 1,200.
Vita vya Israeli dhidi ya Gaza pia vimewaacha zaidi ya asilimia 85 ya idadi ya watu eneo hilo bila makazi yao ya ndani huku kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa, wakati asilimia 60 ya miundombinu ya eneo hilo imeharibiwa, kulingana na UN.
Israel inashutumiwa kwa mauaji ya kimbari na mahakama ya kimataifa ya haki, ambayo, katika uamuzi wa mpito januari hii, iliamuru Tel Aviv kukomesha vitendo vya mauaji ya kimbari na kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa misaada ya kibinadamu inatolewa kwa raia huko Gaza.