Mke wa Rais yuko jijini New York kwa ajili ya mkutano wa 79 wa UNGA, akiwa ameambatana na Rais Recep Tayyip Erdogan./Picha: AA  

Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, katika makao makuu ya Umoja huo jijini New York, kujadiliana masuala ya uhifadhi wa taka ulimwenguni.

Kama mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Watu Mashuhuri la kushughulikia uhifadhi taka, Erdogan aliangazia majukumu ya bodi hiyo, kulingana na malengo ya maendeleo endelevu, alipokutana na Guterres siku ya Jumanne.

Erdogan pia aliangazia ushirikiano wa Uturuki na Azerbaijan katika maandalizi ya mkutano wa 29 wa Mabadiliko ya Tabia Nchi(COP29), ambao utafanyika Baku, Novemba mwaka huu.

Moja ya siku za mada katika COP29 inatarajiwa kuzingatia "Udhibiti Taka," na matukio mbalimbali yanayohusiana yaliyopangwa kuzunguka mpango huo, Erdogan alisema.

Mke huyo wa Rais pia alimkaribisha Guterres kuhudhuria mkutano wa bodi hiyo wakati wa COP29.

Akizungumzia machafuko yanayoshuhudiwa sehemu mbalimbali, Erdogan alionesha kusikitishwa na uharibifu unaotokana na vita, akisisitiza kuwa uharibu huo huathiri asili na mifumo ya ikolojia na hatimaye mabadiliko ya tabia nchi.

Erdogan alizungumzia mafanikio ya majadiliano aliyofanya na Guterres kwenye ukurasa wa X, akionesha utayari kwenye jitihada za udhibiti taka.

TRT Afrika