Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki na Pakistan kujadili kuhusu nafaka, kukabiliana na udhalilishaji wa Quran

Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki na Pakistan kujadili kuhusu nafaka, kukabiliana na udhalilishaji wa Quran

Hakan Fidan na Bilawal Bhutto Zardari wanatoa uungaji mkono kwa mpango wa nafaka wa Bahari Nyeusi, na kuhimiza juhudi kubwa za kidiplomasia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na mwenzake wa Pakistan walifanya mazungumzo ya kidiplomasia / Picha: Jalada la AA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amezungumza na waziri mwenzake wa Pakistan Bilawal Bhutto Zardari, na kujadili jibu la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) dhidi ya kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya Qur'ani, pamoja na kurefushwa kwa mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi, duru za kidiplomasia za Uturuki zimesema.

Zardari, katika ujumbe wa Twitter, alisema alipongeza "jukumu la Ankara katika kufikia makubaliano ya kihistoria ya Ukanda wa Nafaka wa Bahari Nyeusi," na "aliongeza uungaji mkono kamili wa Pakistan kwa juhudi za kimataifa katika kufufua makubaliano" siku ya Jumamosi.

"Pia alionyesha kulaani vikali vitendo vya kudhalilisha Qur'ani Tukufu katika miji kadhaa ya Ulaya na kuazimia kushirikiana na mataifa mengine ya Kiislamu kuzuia matukio kama hayo," aliongeza.

Mapema wiki hii, mkimbizi wa Iraq mwenye makazi yake Uswidi, Salwan Momika, 37, aliikanyaga na kuipiga teke Quran Tukufu, wiki chache tu baada ya kuchoma moto kurasa za kitabu hicho kitakatifu nje ya msikiti wa Stockholm.

Wakati huo huo, Moscow ilijiondoa katika mkataba wa nafaka wa Bahari Nyeusi, ambao ulisimamiwa na Uturuki mwaka jana ili kupunguza athari za vita vya Urusi na Ukraine dhidi ya bei ya chakula duniani.

Makubaliano hayo yalihakikisha kupitishwa kwa usalama kwa zaidi ya tani milioni 32 za nafaka za Ukrain.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa wito kwa mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kurejesha makubaliano hayo na pia kuzitaka nchi za Magharibi kuzingatia matakwa ya Urusi.

TRT Afrika