Mapinduzi ya FETO ya 2016: Jinsi usiku wa giza zaidi Uturuki ulivyotangaza mwamko mpya katika mahusiano na Afrika

Mapinduzi ya FETO ya 2016: Jinsi usiku wa giza zaidi Uturuki ulivyotangaza mwamko mpya katika mahusiano na Afrika

Uturuki inaadhimisha jaribio la mapinduzi lililofeli la mwaka 2016
Miaka saba baada ya jaribio la mapinduzi lililotibuka, demokrasia ya Uturuki inaendesha gari. Picha: AA

Na Ebubekir Yahya

Usiku wa Julai 15, 2016, kundi la upinzani la jeshi lenye utiifu kwa Shirika la Kigaidi la Fetullahist (FETO) lilijaribu kupindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Uturuki.

Siku hii imesalia kama usiku wa giza zaidi katika historia ya kisiasa ya Uturuki.

Hakuna mtu aliyeweza kuelewa ni nini hasa kilikuwa kinaendelea. Magaidi waliingia ndani ya Jeshi, wakifyatua risasi kwa raia ambao walipaswa kuwalinda.

Ndege za kivita ziliruka na kushambulia maeneo ya kiraia kwa saa nyingi, na kuitumbukiza nchi katika maafa.

Katika muda wa usiku mmoja, usaliti wa FETO katika safu ya jeshi ulisababisha raia 249 kuuawa kote nchini.

Wengine 2,196 walijeruhiwa, haswa katika eneo la kibiashara la Istanbul na mji mkuu wa Ankara.

Hali hiyo ilibadilika majira ya saa sita usiku, wakati Rais Recep Tayyip Erdogan alipowasiliana na raia kupitia kituo cha televisheni cha kibinafsi akitumia programu ya mitandao ya kijamii ili kuwafahamisha kile kilichokuwa kikiendelea.

Wimbi liligeuka dhidi ya waliopanga mapinduzi baada ya Rais Erdogan kuwataka watu wake kupigania demokrasia na mustakabali wa Uturuki | Picha: AA

Rais alitoa wito kwa watu wake kuhamasishwa, kuingia mitaani na viwanjani, na kupinga njama za mapinduzi ili kuokoa demokrasia yao na mustakabali wa nchi.

Wito wa Erdogan kwa wananchi ulipoeleweka serikali ilianza kuondoa wanachama wote wa taasisi za umma wanaohusishwa moja kwa moja na wanaounga mkono FETO.

Miaka saba baadaye, demokrasia ya Uturuki inastawi waziwazi na mustakabali wa nchi hiyo unaonekana kuimarika.

Wapangaji wa mapinduzi walishindwa baada ya mapigano ya saa za vita | Picha: AA

Hadithi ya tahadhari kwa Afrika

Tangu upinzani wa umma kukwamisha majaribio ya FETO ya kuunda mapinduzi kwa kujipenyeza ndani ya jeshi, kumekuwa na mabadiliko ya dhana katika sera ya mambo ya nje ya Uturuki, hasa katika suala la jinsi taifa hilo linavyoshirikiana na nchi za Kiafrika.

Wanachama wa FETO walikuwa wamekimbilia nchi mbalimbali duniani baada ya kushindwa kwa uasi, hasa Marekani, ambapo mkuu wa jaribio la mapinduzi ya kundi la kigaidi, Fetullah Gulen, amekuwa akiongoza ibada yake ya ugaidi kwa zaidi ya miongo mitatu.

Nchi za Kiafrika pia zilishuhudia kuhama kwa wanachama wa FETO, wakijiunga na washirika wao katika sehemu hizo za ulimwengu ambapo wanaendesha biashara kwa mashaka, haswa mashule.

Takriban raia 249 waliuawa shahidi na 2,196 kujeruhiwa kote nchini wakati wa jaribio la mapinduzi lililoshindwa |  Picha: AA

Kwa lengo la kulemaza kabisa shirika la kigaidi na kuzuia vyanzo vyake vya mapato, Uturuki ilianza kushirikisha nchi za Kiafrika, ikizionya dhidi ya hatari ya kuwepo kwa makundi ya kigaidi katika maeneo yao.

Mara kadhaa, Rais Erdogan aliwaonya viongozi wa Afrika dhidi ya hatari inayokuja ya uwepo wa FETO katika nchi zao, akisisitiza kwamba mapema au baadaye, kikundi hicho kinaweza kujaribu kile ambalo lilijaribu usiku wa Julai 15, 2016, nchini Uturuki.

Rais wa Uturuki Erdogan ameboresha pakubwa uhusiano wa nchi yake na Afrika | Picha: AA

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki wakati huo, Mevlut Cavusoglu, pia alikutana na wenzake wengi kutoka nchi za Kiafrika, akiwasimulia jinsi FETO ilivyojaribu kupindua demokrasia ya Uturuki, na tishio linalokuja la kupinduliwa sawa na kiota cha ugaidi katika sehemu za dunai ambapo FETO ipo.

Mamlaka ilishauri nchi za Kiafrika kuwafukuza au kuwarudisha wanachama wa FETO, na pia kukabidhi shule zinazoendeshwa na shirika hilo kwa taasisi ya Maarif, asasi ya umma isiyo ya kifaida.

Kukuza uhusiano na Afrika

Juhudi zisizo na kikomo za Uturuki za kukuza uhusiano na ushirikiano na bara la Afrika zimekuwa somo katika sera za kigeni.

Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Uturuki-Afrika mjini Istanbul kuanzia Desemba 17 hadi 21, 2021, ulikuwa na marais kadhaa wa Afrika waliohudhuria.

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Rais Erdogan alitaka ushirikiano zaidi na viongozi wa Afrika, akisisitiza kuwa ilikuwa ni ushindi wa Uturuki na bara zima.

Uturuki inalenga kuongeza kiwango cha biashara na nchi za Afrika hadi dola bilioni 75 | Picha: AA

Taasisi za Uturuki kama vile TIKA, Yunus Emre na taasisi ya Maarif zimetekeleza miradi mingi ya elimu, afya na miundombinu barani Afrika bila kutarajia malipo yoyote.

Uturuki tayari ni nchi ya kwanza duniani katika suala la kupanua misaada ya kibinadamu, ikilinganishwa na pato lake la taifa (GDP).

Ni vyema kutambua kwamba Afrika inafaidika na sehemu kubwa zaidi ya msaada huu.

Nchi za Afrika zimeshuhudia ongezeko kubwa la uwekezaji wa moja kwa moja wa Uturuki, huku makampuni mengi kama hayo yakiweka msingi katika bara hilo. Kiasi cha mtaji wa biashara unaofanywa kati ya Uturuki na Afrika ni zaidi ya dola za Marekani bilioni 30.

Akiwahutubia waandishi wa habari wakati wa Kongamano la Kiuchumi la Uturuki-Afrika Tatu lililofanyika Istanbul kati ya Oktoba 21-22, 2021, Rais Erdogan alisema, "Lengo letu ni kwanza kuongeza kiasi cha dola bilioni 50, na kisha $75 bilioni."

Kumekuwa na mabadilishano ya ziara za manufaa kati ya Rais wa Uturuki Erdogan na viongozi wa Afrika | Picha: AA

Kulingana na Profesa Yunus Turhan, mkurugenzi wa Kituo cha Chuo Kikuu cha Ankara Haci Bayram Veli cha Maombi na Utafiti wa Bonde la Mediterania na Ustaarabu wa Afrika, uthabiti wa juhudi umekuwa msingi wa biashara kati ya Uturuki na Afrika licha ya kupungua kwa kati.

"Mnamo 2013, kiasi cha biashara kilikuwa dola bilioni 21.5; kisha mnamo 2014, iligusa dola bilioni 20.7, na ifikapo 2015, bilioni 18. Mnamo 2016, ilikuwa $17 bilioni, na mnamo 2018, hii iliongezeka hadi $ 22 bilioni. Mnamo 2019, ilikuwa $22.4 bilioni, na mwaka 2020, $22.6 bilioni. Kufikia 2022, kiasi hicho kilifikia zaidi ya dola bilioni 33," anaiambia TRT Afrika.

Kati ya 2016 na 2023, mikutano mingi ya marais, vikao na makongamano ya biashara yameandaliwa kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa Uturuki na Afrika, na kupeleka uhusiano uliopo kwa kiwango cha juu kilicho imarika zaidi, hasa katika kukabiliana na ushindani wa kimataifa ya kuwa na mvuto katika bara la Afrika.

Wakati wa uzinduzi wa TRT Afrika Machi 2023, Jukwaa la Vyombo vya Habari la TRT-Afrika liliandaliwa, ambapo wanachama wa Umoja wa Utangazaji wa Afrika na waandishi wengine wa habari kutoka bara walishiriki.

Uzinduzi wa TRT Afrika mnamo Machi 2023 unaonekana kama hatua kuu katika kukuza uhusiano na bara | Picha: AA

Uzinduzi wa huduma ya kidijitali ya TRT Afrika ili kuonyesha "Afrika kama ilivyo" inaonekana kama hatua ya mabadiliko katika uhusiano wa Uturuki na Afrika.

Huduma hii hutoa habari na vipengele katika lugha nne; Kiingereza, Kifaransa, Kihausa, na Kiswahili.

Ziara ya rais

Rais Erdogan tayari amefanya ziara nyingi zaidi barani Afrika kati ya wakuu wote wa nchi kutoka nje ya bara hilo.

Safari yake ya mwisho barani Afrika ilikuwa Februari 2022, alipotembelea nchi tatu - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal na Guinea-Bissau.

Mnamo Machi 2016, miezi michache kabla ya jaribio la mapinduzi lililoshindwa na FETO, Rais Erdogan alikuwa Equitorial Guinea, Ghana na Nigeria. Mnamo Mei mwaka huo huo, alikuwa ameongoza wajumbe wa biashara na kidiplomasia katika nchi zingine tatu za Afrika - Uganda, Kenya na Somalia.

Ajenda ya ziara hizi ilijikita katika upanuzi wa biashara ya pande zote mbili, mapambano dhidi ya ugaidi, na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

Kuanzia mwaka 2003 hadi sasa, Rais Erdogan ametembelea rasmi zaidi ya nchi 30 za Afrika kwa jumla.

Kuanzia mwaka 2003 hadi sasa, Rais Erdogan ametembelea rasmi zaidi ya nchi 30 za Afrika kwa jumla | Picha: AA

Katika ziara hizi zote, mikataba baina ya nchi na makubaliano ya uwekezaji yanatiwa saini, majukwaa ya biashara na uchumi yanaandaliwa.

Makampuni ya Kituruki na Kiafrika hukutana na kuchunguza njia bora zaidi ya kushirikiana.

Sekta ya ulinzi inayokua

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Uturuki chini ya rais Erdogan imeweka juhudi endelevu ili kuifanya nchi hiyo kuwa huru kutokana na usaidizi wa kigeni katika sekta ya ulinzi.

Msukumo huu wa kupongezwa umesababisha kuimarika kwa sekta ya ulinzi ya Uturuki, ambayo sasa inahesabiwa kuwa miongoni mwa viongozi katika utengenezaji wa vifaa vya kizazi kipya.

Vikosi vya usalama vya Uturuki vinatumia silaha zinazotengenezwa nchini katika kupambana na magaidi ndani na nje ya nchi.

Wakati wanapigana na Daesh na PKK/YPG kaskazini mwa Syria na kaskazini mwa Iraq, vikosi vya Uturuki vilitumia kikamilifu silaha zilizotengenezwa Uturuki.

Baada ya kusambaza vifaa kama hivyo kwa jeshi la Uturuki, tasnia ya ulinzi sasa inasafirisha kwa nchi tofauti kote ulimwenguni.

Hivi majuzi, ulimwengu ulishuhudia utendakazi wa ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB zilizotumiwa na Ukraine dhidi ya Urusi.

Huko Kharabakh, Azerbaijan ilitumia Bayraktar TB2 kuzuia uvamizi wa Waarmenia katika eneo lake. Ndege zisizo na rubani za Uturuki pia zimesaidia nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Libya na Burkina Faso pia katika kukabiliana na ukosefu wa usalama.

Uturuki sasa inaweza kusemekana kuwa inakaribia kujitegemea kikamilifu katika masuala ya vifaa vya ulinzi na programu, na hii ni kwasababu ya mipango ya Rais Erdogan.

Kwa kuzingatia mstari ulioanzishwa wa ushirikiano na Afrika, nchi katika bara hilo haishangazi kuwa mstari wa mbele linapokuja kwenye suala la kuagiza vifaa vya ulinzi kutoka Uturuki.

Uturuki imetia saini itifaki na Makubaliano ya kusambaza silaha za Uturuki kwa angalau nchi 30 za Kiafrika | Picha: AA

Zaidi ya nchi 30 za Afrika, zikiwemo Nigeria, Benin, Chad, Congo, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea-Bissau, Ivory Coast, Kenya, Libya, Mali, Niger, Senegal, Tanzania, Rwanda, Ghana, Madagascar, Sudan, Somalia, Tunisia na Uganda, zimetia saini itifaki na Makubaliano na Uturuki kwa usambazaji wa silaha zinazotengenezwa nchini Uturuki.

Kwa sasa, baadhi ya wafanyakazi wa Jeshi la Anga la Nigeria wanapata mafunzo mjini Ankara kuhusu jinsi ya kuendesha helikopta za T-129 ambazo nchi hiyo ilinunua kutoka TUSAS, kampuni ya kutengeneza ndege za kivita za Uturuki.

Mnamo 2022, Nigeria ilitangaza ununuzi wa helikopta sita za T-129 kutoka TUSAS kama sehemu ya uimarishaji wa usalama unaolenga kumaliza ugaidi katika eneo lake.

Diplomasia angani

Uturuki ina idadi kubwa zaidi ya misheni za kidiplomasia barani Afrika kati ya nchi zilizo nje ya bara hilo.

Kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Uturuki, nchi hiyo kwa sasa ina balozi 12 na jumbe 44 barani Afrika.

Prof. Turhan anahusisha mawasiliano haya na uwiano wa ushirikiano wa pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na ziara za Rais Erdogan barani Afrika na safari za wakuu wa nchi za Afrika kwenda Uturuki, baada ya matukio ya Julai 15, 2016.

Shirika la ndege la Turkish Airlines, pia, limeongeza safari zaidi barani Afrika kwenye mtandao au mzunguko wake, likiongoza orodha ya waajiriwa wa kigeni wanaosafiri kwa ndege kwenda na kutoka barani humo.

Kufikia Mei 2023, Shirika la Ndege la Uturuki lilikuwa na muunganisho wa kwenda na kutoka katika vituo 62 vya kustaajabisha katika nchi 41 za Afrika.

Shirika la ndege la Uturuki limeongeza safari zake hadi kufikia vituo 62 katika nchi 41 za Afrika katika miaka ya hivi karibuni | Picha: AA

Elimu na ufadhili wa masomo

Uturuki inatoa umuhimu mkubwa kwa sera zake za ushirikiano za Kiafrika, ambazo zinaenea hadi kuunda uwanja sawa kwa pande zote.

Prof. Turhan anadokeza kwamba baada ya mapinduzi ya Julai 15, 2016, Uturuki ilibadilisha mwelekeo wake wa Kiafrika na sera zinazozingatia maendeleo ya rasilimali watu.

"Katika jitihada zake za kulemaza shughuli za FETO nje ya nchi baada ya kuzifuta ndani, Uturuki ilianzisha mpango mpya wa utekelezaji ambao ulitambua Afrika kama bara muhimu sana," anaiambia TRT Afrika.

"FETO ingefanya kazi kwa uhuru barani Afrika, na Uturuki ilianza hatua ya kimkakati ya kukomesha shughuli za kundi la kigaidi duniani kote.

Hili lilihusisha kuangazia mashirika yake ya kiraia na shule, ambazo hutumika kama vyombo vya ushawishi kwa shirika hilo katika nchi mbalimbali.

Kundi hilo la kigaidi pia lilifanya propaganda dhidi ya Uturuki kwa njia zote zinazowezekana. Kwa hivyo, Rais Erdogan, wakati wowote anapokutana na viongozi wa Afrika wakati wa ziara zao za pamoja, anajaribu kuvuta hisia zao dhidi ya hatari inayoletwa na FETO.

"Wakati wa ziara ya Rais Erdogan mwaka 2017 katika baadhi ya nchi za Afrika Kusini na Mashariki kama vile Tanzania, Msumbiji na Madagascar, tishio kutoka kwa FETO lilijitokeza kwenye ajenda ya majadiliano.

Kulingana na Prof. Turhan, juhudi za Uturuki za kuwatimua FETO kutoka Afrika huchukua pande nne tofauti. Kwanza na muhimu zaidi ni kuendeleza sekta ya elimu, jambo ambalo ni chanzo kikubwa cha mapato kwa shirika la ugaidi katika nchi za Afrika.

Mnamo Juni 2016, Uturuki ilijumuisha taasisi ya Maarif kufanya kazi ndani na nje ya nchi. Jukumu lilikuwa kwa taasisi hiyo kuchukua shule zote zinazoendeshwa na FETO katika mwambao wa Afrika.

Rais wa Maarif Foundation, Prof Birol Akgun, anaiambia TRT Afrika kwamba sasa inafanya kazi katika nchi 25 za Afrika.

"Katika nchi 15, shule zinazoendeshwa na FETO zimekabidhiwa kwa taasisi."

Maarif Foundation imepata mafanikio makubwa katika kutwaa shule za FETO barani Afrika ikiwemo Tanzania | Picha: AA

Taasisi ya Maarif inachukua shule hizi kwa lengo la kuzikomboa nchi za Kiafrika kutoka kwa hatari inayokuja ya kuwa na FETO kati yao, na pia kuzuia kabisa vyanzo vya mapato vya shirika hilo nje ya Uturuki.

Kwa sera yake ya kimkakati na yenye nguvu, Uturuki inalenga kuendelea kuimarisha uhusiano wake na bara la Afrika katika sekta zote.

Huku Afrika ikiwa uwanja wa ushindani wa kimataifa, Uturuki inahitaji kufanya zaidi ili kudumisha nafasi yake inayostahili katika bara.

Uwekezaji zaidi wa Uturuki unaonekana kuelekea Afrika, hasa katika kilimo, nishati, ujenzi, madini, ulinzi na elimu.

TRT Afrika