Uturuki humchagua rais kupitia mfumo wa raundi mbili huku Wabunge wakichaguliwa kupitia mfumo wa uwakilishi sawia.
1. Mfumo wa uchaguzi wa Uturuki ni mfumo mchanganyiko
Mchanganyiko wa uwakilishi sawia na upigaji kura za wengi. Dhana ya uwakilishi sawia inaruhusu idadi ya viti vinavyoshikiliwa na kundi la kisiasa au chama katika chombo cha kutunga sheria kuamuliwa na idadi ya kura za wananchi zilizopokelewa. Kura nyingi ni halali kwa uchaguzi wa urais na ina maana tu kupata zaidi ya nusu ya mgao wa kura za kitaifa.
Moja ni kumchagua rais na nyingine ni kwa ajili ya kuwapigia kura Wabunge kutoka kila wilaya ya uchaguzi.
3. Sharti la kiwango cha juu:
Ili kuingia bungeni, chama cha kisiasa lazima kipate angalau asilimia 7 ya kura za kitaifa, kulingana na sheria mpya ya uchaguzi iliyopitishwa Aprili mwaka jana. Sheria inaruhusu uundaji wa ushirikiano kati ya vyama tofauti vya kisiasa. Kwa hivyo, chama chochote kinaweza kupata kiti cha ubunge ikiwa kitaunda muungano ambao kwa pamoja hupokea zaidi ya asilimia 7 ya kura katika wilaya yoyote ya Uturuki.
4. Wilaya za kupiga kura:
Kuna wilaya 87 za uchaguzi kote Uturuki. Idadi ya wabunge wanao wakilisha kila wilaya inatofautiana kulingana na uwiano wa watu. Kwa mfano, Istanbul ina wabunge 98 kwa vile ndilo jiji lenye watu wengi zaidi nchini na Ankara ina wabunge 36, huku majimbo ya Tunceli na Bayburt yakiwa na 1 pekee kwa kila moja.
5. Mfumo wa orodha zilizofungwa:
Orodha za vyama vilivyofungwa inamaanisha kuwa mpangilio wa vyeo vya wagombea hauwezi kubadilishwa na wapiga kura husika.
6. Kuchagua rais:
Raia wa Uturuki wanamchagua rais wao tofauti na bunge, kwa kutumia mfumo wa kura mbili za wengi. Iwapo hakuna mgombeaji atashinda kura nyingi katika duru ya kwanza, wagombeaji wawili wa juu hushindana katika duru ya pili ya upigaji kura ambapo mgombea mmoja anafaa kupata zaidi ya asilimia 50 ili kuchaguliwa.