Vifaa hivyo viliwasilishwa kwa jeshi la Mali siku ya Jumanne. Picha: Wingine

Mali imenunua zana mpya za kijeshi, zikiwemo ndege zisizo na rubani kutoka Uturuki, ili kuimarisha mapambano yake dhidi ya makundi yenye silaha.

Rais wa mpito wa Mali, Jenerali Assimi Goita, aliwasilisha magari mapya ya kubeba ndege kwa Wanajeshi wa Mali (FAMa) mjini Bamako siku ya Jumanne, kupitia Wizara ya Ulinzi na Masuala ya Maveterani, kulingana na TV ya serikali.

Vifaa hivi vya kisasa vinalenga kuimarisha vita dhidi ya ugaidi na kuimarisha usalama wa taifa.

Vifaa hivyo ni pamoja na ndege isiyo na rubani ya AKINCI, inayotengenezwa na kampuni ya Uturuki ya Baykar, inayojulikana kwa ndege yake mashuhuri ya TB2.

Kipaumbele cha juu

Waziri wa Ulinzi wa Mali, Jenerali Sadio Camara, alipongeza hatu hizo. ‘’Kwa ndege hizi mpya zilizopatikana kutoka kwa bajeti ya taifa, tunachukua mkondo mpya. Zitasaidia kuimarisha eneo la taifa na kupunguza vitisho vya magaidi popote walipo," alisema.

"Tunawashukuru kwa kuendelea kusikiliza kwa watu wa Mali, mamlaka za juu zaidi zimeweka urejeshaji wa usalama katika vipaumbele vya juu," Jenerali Camara aliongeza.

Waziri wa ulinzi alivihimiza vikosi vya usalama kutumia vifaa hivyo ipasavyo ili kukidhi matarajio ya watu wa Mali wakati nchi hiyo ikikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya watu wanaotaka kujitenga wanaoongozwa na Tuareg na makundi mbalimbali ya kigaidi.

Kuboreka kwa mahusiano

Afisa wa jeshi la Mali alielezea ndege hiyo kama "kifaa cha kweli cha mapigano'', na alionyesha matumaini kufuatia kukabidhiwa kwa kifaa hicho.

‘’Ikiwa na kamera za hali ya juu, ndege isiyo na rubani ya AKINCI inahakikisha maono ya mchana na usiku, ikiwa na uwezp wa kufuatilia eneo lote la kitaifa,” afisa huyo aliongeza.

Kuongezeka kwa uhusiano wa Uturuki na eneo la Sahel, haswa na Niger, Mali, na Burkina Faso, kumesababisha kuongezeka kwa ushirikiano wa kiuchumi na kijeshi.

Haya yanajiri huku nchi za eneo hilo zikikata uhusiano na madola ya Magharibi, akiwemo mtawala wa zamani wa kikoloni, Ufaransa. Mara nyingi wanaelezea Uturuki kama mshirika wa kuaminika.

TRT Afrika