Chini ya mada kuu "Kuinua Diplomasia Katikati ya Migogoro," kongamano hilo linaangazia masuala mbalimbali ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mgogoro wa hali ya hewa, uhamiaji, kuongezeka kwa hisia dhidi ya Uislamu, vita vya kibiashara, na akili bandia.
Utamaduni wa Kiafrika unaonyeshwa katika mkutano wa kimataifa wa kidiplomasia , yaani Antalya Diplomacy Forum inayofanyika mjini Antalya nchini Uturuki .
Huku viongozi wa tabaka mbali mbali wa dunia wakikutana kujadili maswala nyeti yanayoathiri dunia wakati wa sasa, maonyesho haya yanaelea Afrika kupitia vyombo hivi vilivyopangwa katika kiingilio kikuu cha mkutano huo .
Vitu aina tofauti vinaashiria jamii tofauti barani , na wengi wanatembelea kituo hiki wakifurahishwa sana na kile ambacho wanasema ni urithi wa kiasili.
Vyombo hivi vinatumika na jamii tofauti barani Afrika kwa ajili ya kuhimiza utamaduni na vingine kwa ajili ya urembo.
Waafrika waliohudhuria mkutano huu mjini Antalya wanaweza kutambua vifaa ambavyo ni vya asili yao , na wengine wanasimama hapa na kujitolea kuelezea watu wengine kuhusu umuhimu wao.