Waumini wa Kiislamu wakishiriki sala ya Eid katika Msikiti Mkuu wa Ayasofya mjini Istanbul. /Picha: AA

Waislamu kote duniani, wakiwemo wa Uturuki wanasheherekea sikukuu ya Eid al Fitr, yenye kuashiria hitimisho la mwezi mtukufu wa Ramadhan, ambapo waumini wengi walikuwa kwenye mfungo.

Siku hii huanza na sala maalumu ya asubuhi, kutembelea ndugu, jamaa na marafiki ambazo huambatana na sherehe mbalimbali ikiwemo kuwapa watoto na watu wengine zawadi.

Watu walidamkia misikitini asubuhi na mapema kukaribisha Eid al Fitr kwa sala.

Kutoka pande tofauti za Istanbul, waturuki wengi na raia wa kigeni walifanya sala ya Eid ndani ya misikiti mkubwa na ya kihistoria mjini hapa. Kati ya misikiti hiyo ni pamoja na msikiti mkuu wa Ayasofya, Suleymaniye na Sultanahmet.

Peremende pamoja na chokoleti ziligawiwa kwa watu mbalimbali kati misikiti hiyo.

Hizi ni baadhi ya picha za shamrashamra za Eid nchini Uturuki.

AA.

Eid al Fitr, ambayo hutafsiriwa kama 'sikukuu ya kufuturu', huashiria mwisho wa mwezi wa mfungo, ambao huchukua kati ya siku 29 au 30.

AA.

Eid hutangazwa mwanzoni mwa mwezi wa kumi wa kalenda ya Kiislamu iitwayo Shawwal, unaofuata mwezi wa Ramadhan. Kwa hiyo kuuona mwezi ni muhimu katika kutangaza mwanzo wa mwezi mpya wa mwandamo.

AA.

Kila mwaka, Ramadhani huanza takriban siku kumi mapema kwa sababu mwaka wa mwandamo ni mfupi kuliko mwaka wa jua.

AA.

Quran iliteremshwa kwa mara ya kwanza kwa Mtume Muhammad, ambaye Waislamu wanamwona kama Mtume wa mwisho na ambaye wanamheshimu kwa kuongeza neno 'amani iwe juu yake' katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

AA.

Waislamu husherehekea sikukuu ya Eid kama shukran kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwajaalia kumaliza na kuweza kutimiza wajibu wao kwa kufunga, kukamilisha mambo ya kheri katika mwezi ambao Waislamu wanaona kuwa ni bora kuliko miezi 1,000.

AA.

Waislamu kwa kawaida hutumia tukio hilo kuthibitisha uhusiano wa kifamilia na jumuiya.

AA.

Kufunga wakati wa Ramadhani ni moja ya nguzo tano za Uislamu, pamoja na tamko la Kiislamu la imani, sala ya kila siku, hisani na kutekeleza ibada ya Hija Makka.

TRT Afrika