Upigaji kura nchini Uturuki umeratibiwa kuanza saa 8 asubuhi saa za ndani (0500GMT) na kumalizika saa 11 jioni (1400GMT) mnamo Mei 14. / Picha: AA

Wapiga kura wataweza kupiga kura katika ofisi 177 za wawakilishi katika nchi 74 hadi Mei 9 kati ya saa 3 asubuhi na 3 usiku kwa saa za nchi mwenyeji, siku za kazi na wikendi, kwa mujibu wa Baraza Kuu la Uchaguzi la Uturuki.

Katika miji iliyo na balozi ndogo za Uturuki, upigaji kura utafanyika kati ya 3:00 asubuhi na 10:00 jioni kwa saa za nchi mwenyeji.

Pia, wapiga kura wataweza kupiga kura katika ofisi zozote zilizoteuliwa na balozi ambapo masanduku ya kura yamewekwa, bila kulazimika kufanya miadi ya zoezi hilo.

Ikitokea hakuna mgombea hata mmoja amepata zaidi ya asilimia 50 ya kura, italazimika kuingia katika duru ya pili upigaji kura Mei 28, Mei 20-24 katika ofisi maalum za mwakilishi.

Upigaji kura utafanyika katika ofisi 26 za ubalozi nchini Ujerumani, na ofisi tisa za ubalozi nchini Marekani na Ufaransa.

Karibu Waturuki milioni 6.5 wanaishi katika nchi zingine. Miongoni mwao, milioni 3.28 wana vigezo vya kupiga kura katika uchaguzi ujao wa urais na ubunge.

Ikilinganishwa na wapiga kura milioni 60.9 waliojiandikisha ndani ya Uturuki, kura za Waturuki wanaoishi nje ya nchi zinaweza kuonekana kuwa chache. Lakini katika kinyang'anyiro kikali ambapo kila kura inahesabiwa, muhuri wao wa kuidhinisha unaweza kuwa na matokeo madhubuti, kama ilivyoonekana katika uchaguzi wa 2018 ambao ulipelekea ushindi wa Erdogan.

Miongoni mwa wengi wanaoishi nje ya Uturuki wako Ulaya Magharibi, ambapo wafanyakazi wa Kituruki waliishi tangu miaka ya 1960 kama sehemu ya mpango wa ujenzi wa baada ya Vita vya pili vya dunia. Wanaunda kundi moja kubwa zaidi la wahamiaji Waislamu katika Ulaya Magharibi.

Waturuki walirudi nyumbani kutoka nje walipiga kura zao katika uchaguzi wa kitaifa kwa mara ya kwanza wakati wa uchaguzi wa urais wa Agosti 2014 huku Erdogan akishinda kwa asilimia 62.2 ya kura.

Kwa mujibu wa sheria, kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea, aliyejiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura inayoratibiwa na ofisi za usajili wa idadi ya watu au balozi za kidiplomasia, anastahili kupiga kura.

Ujerumani inaongoza kwa kuwa na orodha kubwa ya wapiga kura milioni 1.4 kutoka Uturuki. Pia ni Ujerumani ambapo siasa za Uturuki zinafanyika kwa kiwango kubwa, ikifuatiwa na Ufaransa, Uholanzi na Ubelgiji.

TRT World