'Janga la karne limeleta hasara ya moja kwa moja ya Dola Bilioni 104, na isiyo ya moja kwa moja ya Dola Bilioni 150: Erdogan

'Janga la karne limeleta hasara ya moja kwa moja ya Dola Bilioni 104, na isiyo ya moja kwa moja ya Dola Bilioni 150: Erdogan

Janga hilo liligharimu zaidi ya maisha ya watu 50,000 na kuwaacha takribani watu milioni 14 nchini Uturuki.
Jumla ya majimbo 11 nchini Uturuki, yakiwemo Adana, Adiyaman, Diyarbakir, Elazig, Hatay, Gaziantep, Kahramanmaras, Kilis, Malatya, Osmaniye, na Sanliurfa, yalikumbwa na matetemeko hayo yenye nguvu ya 7.7 na 7.6, mwezi Februari 2023./Picha: AA 

“Janga la karne” limeisababishia Uturuki hasara ya moja kwa moja ya Dola za Kimarekani Bilioni 104, amesema Rais Erdogan wakati akizungumzia matetemeko pacha ya mwaka 2023.

‘Janga hilo la karne’ limesababisha hasara ya Dola Bilioni 104 na nyingine isiyo ya moja kwa moja ya Dola Bilioni 150 kwa nchi yetu,” alisema Erdogan siku ya Alhamisi wakati wa kumbukumbu maalumu ya matetemeko pacha ya Februari 6, iliyofanyika katika jimbo la Adiyaman.

“Kufikia mwisho wa mwaka, tutakuwa tumejenga jumla ya nyumba 453,000, ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayekosa nyumba wala sehemu ya kufanyia kazi,” aliongeza.

Majimbo 11 yaathirika

"Ndani ya miaka miwili, tumechukua hatua madhubuti ya ujenzi na ukarabati wa maeneo yaliyoathirika, kitu ambacho kisingewezekana kufanywa na nchi nyingine duniani," alibainisha.

Jumla ya majimbo 11 nchini Uturuki, yakiwemo Adana, Adiyaman, Diyarbakir, Elazig, Hatay, Gaziantep, Kahramanmaras, Kilis, Malatya, Osmaniye, na Sanliurfa, yalikumbwa na matetemeko hayo yenye nguvu ya 7.7 na 7.6, mwezi Februari 2023.

Matetemeko hayo yaliua watu wapatao 53,537 na kujeruhi zaidi ya 107,000, na hivyo kuathiri maisha ya watu zaidi ya milioni 14.

TRT Afrika