Uturuki yapuuza 'madai yasiyokuwa na msingi' ya Netanyahu dhidi ya Rais Erdogan. / Picha: AA

Serikali ya Uturuki imepinga "uchongezi usio na msingi " uliofanywa na waziri mkuu wa Israeli dhidi ya Rais Recep Tayyip Erdogan, huku ikisema maafisa wa Israeli" hawana haki ya kuzungumza juu ya sheria."

"Maafisa wa Israeli, ambao wameingia katika kurasa za giza za historia na ukandamizaji na mauaji yaliyofanywa dhidi ya Wapalestina, hawana haki ya kuzungumza juu ya sheria," Wizara ya Mambo ya Nje ilisema katika taarifa iliyotumwa Jumatano.

Benjamin Netanyahu "(Waziri Mkuu wa Israeli) na Eli Cohen (Waziri wa Mambo ya Nje), ambao wote hawana furaha na ukweli unaoonyeshwa, hawataweza kuficha uhalifu wao wenyewe na kashfa zao zisizo na msingi kwa Recep Tayyip Erdogan, rais wa Jamhuri ya Uturuki," iliongeza.

Wachochezi na wahusika wa uhalifu dhidi ya binadamu, uliosababisha chuki kubwa miongoni mwa mawazo ya umma duniani, hivi karibuni au baadaye watahukumiwa, Wizara ilisisitiza.

"Utawala wa Israeli, ambao tayari umepoteza uhalali wake katika dhamiri ya binadamu, hawataweza kuficha uhalifu walioufanya kwa kulipua hospitali na kuua wanawake na watoto mbele ya ulimwengu wote na hawataweza kugeuza umakini," ilisema.

Uturuki itaendelea kusimama dhidi ya mauaji huko Gaza, Palestina na kuunga mkono haki za watu wa Palestina, Wizara imeongeza.

TRT World