Israeli imeziteka taasisi zote zenye majukumu kulinda amani, haki za binadamu na demokrasia, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.
"Serikali ya Israeli inapofushwa na kiina macho cha Kisayuni, imeziteka taasisi zote za kulinda amani, haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari na demokrasia, sio Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa," alisema Rais Erdogan alisema siku ya Jumatano jijini Ankara.
"Mauaji ya kimbari ya Gaza yameondoa vificho vyote duniani. Kupuuza kwa utawala wa Israeli kwa sheria hiyo kwa mara nyingine tena kumetukumbusha kwamba maadili ambayo nchi za Magharibi zilidai kuwa zinatetea kwa miongo kadhaa ni tupu kabisa. Sote tunaona kwamba kile wanachokiita ustaarabu si chochote ila ni jini lisilo na meno.”
"Lazima nieleze ukweli ufuatao ingawa unagusa moyo wangu: Ulimwengu wetu wa Kiislamu, ambao idadi yake inakaribia bilioni 2, kwa bahati mbaya, imefanya vibaya katika jaribio la Gaza na Lebanon. Hatukuweza kuwazuia ndugu na dada zetu 50,000 wasisambaratike katika mauaji ya utawala wa Kisayuni.”
Erdogan amelaani ukimya wa jumuiya kimataifa kuhusu mgogoro wa Gaza, na kuutaja kuwa ni "aibu" kwa binadamu huku raia wakikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara na hali mbaya zaidi katika eneo la Palestina.
Hakuna hatua za kuzuia zinazochukuliwa kumkomesha "adui wa ubinadamu, (Rais wa Israeli) Netanyahu," aliongeza, akiita hali hiyo "anguko la ubinadamu."
Kando na nchi chache, hakuna hisia kali kuhusu Gaza kutoka kwa ulimwengu wa Kiislamu, alisema Rais wa Uturuki, na kuongeza kuwa kutochukua hatua huko "kumeandikwa katika historia."
"Tuna wajibu kwa ndugu zetu wa Gaza ambao wanachomwa moto wakiwa hai, wakiuawa shahidi kwa mabomu ya wahalifu wa Kisayuni kwenye mahema waliyokuwa wakiishi," kiongozi huyo wa Uturuki alisema.
Erdogan pia alionya kwamba Israeli itawaweka watu milioni 2 kwenye "kama kambi ya Wanazi" wanaoteseka msimu huu wa baridi, akihimiza hatua ya "kuzuia ubinadamu kugonga mwamba."
Jeshi la Israeli limeendelea na mashambulizi makubwa huko Gaza tangu uvamizi wa mpaka wa kundi la wapiganaji wa Palestina la Hamas Oktoba mwaka jana, licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano.
Katika zaidi ya mwaka mmoja, mashambulizi ya Israeli yameua zaidi ya watu 43,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi zaidi ya 101,000, kulingana na mamlaka ya afya ya eneo hilo.
Mashambulizi ya Israeli yamewafanya takriban wakazi wote wa eneo hilo kuhama makazi yao huku kukiwa na mzingiro unaoendelea ambao umesababisha uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa.
Israeli pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwa hatua zake huko Gaza.