Gaidi wa PKK anayehusishwa na tukio la TUSAS akamatwa Italia

Gaidi wa PKK anayehusishwa na tukio la TUSAS akamatwa Italia

Gaidi wa PKK Velat Cetinkaya ni kati ya watuhumiwa wanaohusishwa na tukio la TUSAS.
Gaidi wa kikundi cha PKK, Velat Cetinkaya amehamishiwa kwenye gereza la Regina Coelli, lililopo jijini Roma./Picha: AA

Mamlaka za nchini Uturuki zinamshikilia gaidi wa PKK Velat Cetinkaya mjini Roma, baada ya kutambulika kama mmoja ya washukiwa wa tukio la kigaidi lililotokea mwezi Oktoba katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, kulingana na vyombo vya habari vya Uturuki na Italia.

Gaidi huyo alikamatwa katika eneo la Campino, ambalo lipo kilomita zipatazo 30 kutoka jiji la Roma, baada ya kutolewa kwa kibali cha kumkamata miaka miwili kabla. Mamlaka za Ujerumani zinamtuhumu Cetinkaya kwa ugaidi, huku mahakama ya Stuttgart ikitoa amri ya kukamatwa kwake mwaka 2022.

Polisi walimkamata Cetinkaya katika nyumba ya kupanga ambayo hutumiwa na watalii. Uwepo wake katika eneo hilo unatokana na msako mkali uliofanywa kwenye mahoteli na nyumba za wageni, ukitekelezwa mara baada ya kutokea kwa tukio la kigaidi katika kampuni ya anga na vifaa vya usalama ya TUSAS jijini Ankara siku ya Oktoba 23.

Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine 22.

Cetinkaya amehamishwa kwenye gereza la Regina Coeli. Kulingana na msemaji wa jeshi la polisi, msako huo uliendeshwa kwa ushirikiano wa maafisa kutoka taasisi ya ushirikiano wa polisi.

Mamlaka zinaendelea na uchunguzi wa vitendo vya Cetinkaya na uhusiano wake wakati yuko Roma, na iwapo kuwa msaada wowote alikuwa akipokea.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kuwa Cetinkaya ni kati ya wahusika wakuu wa shambulio la TUSAS.

Siku ya Oktoba 23, magaidi wawili wakiwa na silaha walivamia eneo la maegesho la teksi ambalo walilitwaa mara baada ya kumuua mmoja wa madereva na kufanya mashambulizi.

Kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya, wahusika hao ni wanachama wa kikundi cha PKK, kilichoainishwa kama kikundi cha kigaidi katika nchi za Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya.

Uturuki iliongeza udhibiti wa shughuli za magaidi wa PKK katika eneo la Iraq na Syria.

TUSAS inahusika na utengenezaji wa vifaa vya ulinzi kama vile ndege za kijeshi, ndege zisizo na rubani na mitambo ya anga.

TRT Afrika