Na Yusuf Kamadan
Shirika la kigaidi la Fetullah (FETO), linaloongozwa na Fetullah Gulen aliyekimbia uhamishoni, limekuwa likijificha kwenye mwamvuli wa utoaji elimu na misaada ya kibinadamu.
Ndio, ushahidi unaonesha kuwa shirika hilo linafanana na vuguvugu la Osho la miaka ya 80.
Kama ilivyokuwa kwa Rajneeshpuram, ambaye alitumia dini kama kificho cha kutekeleza uhalifu na utakatishaji fedha, FETO imejijenegea himaya kubwa, hususani nchini Marekani.
Hata baada ya kifo cha Gulen mwaka 2024, shirika hilo bado linaendelea kufanya kazi nchini Marekani, likijikita kupitia mitandao tofauti. Chini ya mwamvuli wa shule na vikundi mbalimbali.
Uhusiano na vuguvugu la Osho
Ni dhahiri kuwa FETO ni kikundi hatarishi, huku wanachama wake wakiaminishwa kuwa Gulen hakuwa na kosa lolote na wanapaswa kupokea maagizo kutoka kwake.
Kama ilivyokuwa kwa vuguvugu la Osho na vitendo vyao vya shuruti, FETO imetuhumiwa kwa kutumia hadaa za kisaikolojia ili kudhibiti wanachama wake.
Lengo kuu la taasisi hiyo ni kujipenyeza ndani ya taasisi na kukamata dola, kama walivyojaribu kufanya wakati wa jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa ya mwaka 2016 nchini Uturuki.
Taswira ya ndani ya kikundi hicho inaakisi vuguvugu la Osho.
Kama tu ilivyokuwa kwa Rajneeshpuram, ajenda ya uhalifu ya FETO nayo imewekwa wazi.
Shule kama mwamvuli wa rushwa
Nchini Marekani, FETO inasimamia mtandao wa shule zaidi ya 50.
Kama tu intelijensia ya Uturuki ilivyoweka wazi, shule hizi, ambazo hutumia majina yasiyo rasmi kuficha uhusiano wao na Gulen, zimeghubikwa na utata.
Moja ya mbinu zinazotumika na FETO ni pamoja na mpango wa Visa wa H-1B.
Mamia ya wanachama wa shirika hilo, wengi wakiwa hawana vigezo, wamepelekwa Marekani kufundisha shule mbalimbali na kushika nafasi za kiutawala.
Inadaiwa kuwa, waajiriwa hawa wanalazimika kutoa sehemu ya mishahara yao kwa shirika la FETO, ili kufanikisha shughuli za mtandao huo ulimwenguni.
Mbali na hayo, shule zinazoendeshwa na FETO zimehusishwa kwenye zabuni za kughushwa, na hivyo kufanikisha shughuli zao kupitia fedha zilizopatikana isivyo halali.
Katika ripoti yake ya mwaka 2019, taasisi ya Forbes iliangazia matumizi hayo mabaya ya fedha yenye kuweka bayana namna fedha za walipa kodi zinazotumika kusukuma shughuli za mtandao huo.
Utafiti huo unafanana kabisa na kile kilichokuwa kinafanywa na vuguvugu la Osho
Tishio kwa usalama wa taifa?
Shughuli za FETO zinaenda zaidi ya elimu. Taasisi hiyo imekuwa ikijepenyeza kupitia mashirika mbalimbali ya kisera nchini Marekani.
Mara kwa mara, limekuwa likijitambulisha kama mwathirika wa mateso ya kisiasa kutoka Uturuki, na hivyo kukwepesha ukweli halisi.
Hali hii, inaweka usalama wa taifa rehani.
Kwa kutumia vibaya mifumo ya fedha na ya kisheria nchini humo, FETO imeshusha uaminifu wake kwa umma.
Upinzani wa FETO kwa Trump
Kujihusisha kwa FETO katika siasa za Marekani kunaenea hadi kwenye kampeni zinazolengwa dhidi ya watu binafsi inaowaona kama vikwazo kwa ajenda yake.
Rais Donald Trump, amekuwa akilengwa mara kwa mara na wafuasi wa FETO.
Kwa mfano, mwezi Agosti mwaka 2024, kupitia chapisho lake, Ergun Babahan, aliandika , "Trump amechanganyikiwa, atashindwa vibaya kwenye uchaguzi."
Dharau ya Babahan kwa Trump imenakiliwa vizuri tu, likiwemo chapisho lake la mwaka 2023 alivyodai, "Majaji wahafidhina walioteuliwa na Trump wanaimaliza Marekani," na ile nyingine ya mwaka 2020 ambayo ililalamikia jaribio la Trump kuwa na ushawishi wakati wa kuhesabu kura, akiuita "fedheha kwa historia ya demokrasia ".
Kwa upande wake, mwanachama mwingine wa FETO Kuzzat Altay, alisema, "Trump ndiye rais dikteta zaidi kuwahi kutokea," huku Nedim Hazar akidai, "Kwa Trump, athari za ufashisti duniani zitafikia kilele!"
Pia kuna machapisho ya Said Sefa aliyemuelezea Trump kama "jogoo" na akaelezea urais wake kama "chanzo cha wajinga na mafashisti".
Sevgi Akarcesme hakuwa mbali na maoni hayo, baada ya kumwita Trump "mtu mwenye ubinafsi ambaye anaendelea kudhoofisha demokrasia kwa njia za kidemokrasia".
Mwandishi mshirika wa FETO Ugur Tezcan aliandika katika makala, "Viongozi wote wa kiimla na wafuasi wao, duru za mrengo wa kulia na za kifashisti kote ulimwenguni zinasubiri kwa hamu urais mpya wa Trump."
Wakati huo huo, Adem Yavuz Arslan amekuwa akimshambulia Trump mara kwa mara katika machapisho na matangazo yake, akiangazia zaidi upinzani wa FETO kwa rais wa Marekani.
Umuhimu wa tahadhari
Uwepo wa kikundi cha FETO nchini Marekani ni mfano hai wa namna taasisi zinavyoweza kutumia mifumo ya kidemokrasia kwa faida yao.
Licha ya kujikita katika kukuza elimu na dini kwa taswira ya nje, bado kundi hili linajipambanua na ufisadi, upotoshaji na ulaghai.
Ili kulinda rasilimali za umma na usalama wa taifa, mamlaka za Marekani lazima zifuatilie kwa karibu shughuli za FETO na kuiwajibisha shirika kwa makosa yake.
Kwa kutambua uwiano wake na madhehebu mengine na matamshi yake thabiti dhidi ya Trump, watunga sera wanaweza kuelewa vyema nia ya kweli ya FETO na kuchukua hatua zinazofaa ili kuzuia unyonyaji.
Vitendo vya FETO viwe ni kama onyo la hatari ya mamlaka iliyo huru, ikisisitiza umuhimu wa kuwa macho katika kulinda maadili ya kidemokrasia.