Kikosi cha timu ya Uturuki kinachoshiriki michuano ya EURO 2024./Picha: Getty

Timu ya taifa ya Uturuki inaingia uwanjani inajitupa uwanjani usiku wa Juni 26, 2024 kumenyana na Czechia katika mchezo wa mwisho wa kundi F, katika uwanja wa Volksparkstadion, mjini Hamburg nchini Ujerumani.

Uturuki inasaka ushindi wa pili katika kundi hilo, baada ya kufanya vizuri katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Georgia uliofanyika Juni 18, ambapo timu hiyo ilivuna alama tatu kufuatia ushindi wa 3-1.

Hata hivyo, timu hiyo ilipoteza mchezo wake wa pili dhidi ya Ureno, baada ya kukubali kufungwa mabao 3-0, mchezo uliochezwa Juni 22, 2024.

Kikosi cha Uturuki, kinachofundishwa na Mtaliano Vincenzo Montella, kitakuwa kinasaka ushindi ili kiweze kuingia hatua ya mtoano ya mashindano hayo makubwa barani Ulaya.

Uturuki itakuwa inategemea huduma za nahodha Hakan Çalhanoğlu kinda nyota Arda Güler, kuweza kutinga hatua ya makundi katika michuano ya EURO 2024.

TRT Afrika