Maendeleo ya hivi karibuni nchini Syria yanaonesha ufanisi wa sera ya nje ya Uturuki, alisema Rais Recep Tayyip Erdogan, akisisitizia umuhimu wa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya katika kukabiliana na ugaidi na ujenzi mpya wa Syria.
Erdogan alikuwa mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Hungaria Viktor Orban katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara siku ya Alhamisi, kujadiliana uhusiano wa nchi mbili, masuala ya kikanda nay a kiulimwengu, kulingana kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.
Rais Erdogan alisisitiza utayari wa Uturuki wa kuimarisha uhusiano wake wa miaka 100 na Hungaria, akisema kuwa uko kati katika hatua nzuri.
Aligusia pia umuhimu wa kukuza jitihada za pande zote mbili za kuongeza kiwango cha biashara hadi kufikia dola bilioni 6.
Kulingana na Rais Erdogan, Ankara na Budapest zina nia ya kuimarisha uhisiano mzuri kati yao, uliozidi miaka 100, akisisitizia umuhimu wa kukuza juhudi za kuongeza kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili hadi kufikia dola bilioni 6.
Erdogan alielezea furaha yake ya kuwa mwenyeji wa Waziri Mkuu Orban na ujumbe wake kwenye hafla ya kuhitimisha mwaka wa 2024 wa kitamaduni wa Uturuki na Hungaria.
Alielezea pia matamanio ya kuongeza ushirikiano katika nyanja mbalimbali, hususani nishati.