Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa kutekeleza usitishwaji wa ugawaji wa silaha kwa Israeli utaongeza shinikizo kwa Tel Aviv kusitisha mashambulizi dhidi ya Gaza na Lebanon.
“Rais Erdogan alisisitiza ulazima wa kuiwekea Israeli zuio hilo kama namna ya kuongeza shinikizo kuwa mpango wa kuiwekea Israeli shinikizo,” ilisema Kurugenzi ya Mawasiliano katika ukurasa wa X kufuatia kikao chake na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Ahmed Aboul Gheit siku ya Jumatano.
Aliongeza kuwa Tel Aviv inajaribu kueneza "mioto ya migogoro" ambayo imeiwasha sehemu zote za Mashariki ya Kati, wakiwa na nia ya kuwaacha Wapalestina bila makazi katika ardhi yao wenyewe.
“Wakati wa kikao hicho, masuala ya kikanda na ya ulimwengu, likiwemo suala la mashambulizi ya Israeli dhidi ya maeneo ya Palestina na Lebanon,” iliongeza.
Alisisitiza kuwa Ankara itaendelea kutafuta kila njia kuhakikisha kuwa "Israeli inawajibishwa kwa makosa yake."
Aidha, Erdogan alieleza matumaini ya Uturuki kwamba mivutano nchini Syria, Libya, Somalia na Ethiopia itatatuliwa haraka, na kuruhusu maeneo hayo kupata amani na utulivu.