Rais wa Uturuki Achukua Hatua Katika Mkutano wa NATO: Asukuma Njia ya Umoja wa Ulaya Kuhimiza ombi la Uswidi kujiunga na NATO / Picha: Jalada la Reuters

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema kuwa atahimiza mkutano wa NATO kufungua njia ya uanachama wa Ankara katika Umoja wa Ulaya ili Uturuki ifungue njia kwa uanachama wa Uswidi kwa NATO.

"Ninatoa wito kwa nchi ambazo zimeiweka Uturuki ikisubiria kwenye lango la EU kwa zaidi ya miaka 50," Erdogan alisema Jumatatu kabla ya kuondoka kuelekea mji mkuu wa Lithuania, Vilnius, kuhudhuria mkutano wa NATO.

"Kwanza, hebu tufungue njia kwa Uturuki katika EU, na kisha tutafungua njia kwa Uswidi kama tulivyoifanyia Finland."

Erdogan pia alikariri kwamba uanachama wa NATO wa Uswidi unategemea utimilifu wa masuala yaliyotajwa katika makubaliano ya mwaka jana ya pande tatu yaliyotiwa saini mjini Madrid wakati wa mkutano wa wa NATO.

Hapo awali Erdogan alikuwa ameeleza kusikitishwa na kile anachokiita kushindwa kwa Uswidi kutimiza ahadi yake ya kukabiliana na magaidi wa PKK na wafuasi wake "wanaozurura katika mitaa" ya Stockholm.

Uturuki iliomba kwa mara ya kwanza kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya - iliyotangulia muungano wa EU - mnamo 1987.

Iliwekwa katika orodha ya walioomba kujiunga na EU mnamo 1999 na ilizindua rasmi mazungumzo ya uanachama na umoja huo mnamo 2005. Mazungumzo hayo yalikwama mnamo 2016 kutokana na sababu mbali mbali.

Suala la Ukraine kutawala mkutano wa NATO

Mkutano wa siku mbili wa viongozi wa NATO unaoanza Julai 10 utashughulikia mzozo unaoendelea kati ya Urusi na Ukrain, changamoto zake kwa NATO, na hatua za kuimarisha ulinzi na kukinga mashambulio ya kijeshi. Jitihada za Uswidi kujiunga na NATO pia zitakuwa kwenye ajenda.

Kando ya mkutano huo, Erdogan anatarajiwa kufanya mikutano ya pande mbili na viongozi wenzake akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden.

Finland na Uswidi ziliomba uanachama wa NATO mara tu baada ya kuanza kwa mzozo kati ya Urusi na Unkrain mnamo Februari 2022. Ingawa Uturuki iliidhinisha uanachama wa Finland katika NATO, inasubiri Uswidi kutimiza ahadi zake chini ya makubaliano ya mwaka jana ya pande tatu yaliyotiwa saini huko Madrid wakati wa mkutano wa NATO. .

Hapo awali, Erdogan alisisitiza kwamba Uswidi haiwezi kuwa na matumaini ya kujiunga na NATO ilimradi inatoa makazi na uhuru kwa magaidi na wafuasi wa wao.

Ili kujiunga na NATO, Uswidi inahitaji idhini ya wanachama wake wote wa sasa, pamoja na Uturuki, ambayo imekuwa katika muungano huo kwa zaidi ya miaka 70 na inajivunia jeshi lake la pili kwa ukubwa.

TRT World