Rais wa Türkiye Tayyip Erdogan akutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas na kiongozi mkuu wa Hamas wa kundi la Palestina Ismail Haniyeh katika Ikulu ya rais mjini Ankara, 2023. / Picha: Reuters 

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikutana na rais wa Palestina Mahmoud Abbas pamoja na Ismail Haniyeh, kiongozi wa kundi la Palestina Hamas mjini Ankara siku ya Jumatano, ofisi ya Erdogan ilisema.

Abbas amefanya ziara ya Uturuki na hapo awali alikutana na Erdogan siku ya Jumanne.

Abbas na Haniyeh hawajaweza kutatua mzozo wao tangu mwaka 2007, wakati Hamas, ambayo inapinga mapatano ya amani na Israel, katika udhibiti wa Gaza iliyozingirwa.

Mamlaka ya Palestina ya Abbas bado inatawala katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel.

Siku ya Jumanne, Abbas alikubaliana na Haniyeh, ambaye kwa sasa anaishi kati ya Qatar na Uturuki, kufanya mkutano mkubwa kuhusisha makundi katika mji mkuu wa Misri, Cairo, mwishoni mwa Julai, kujadili mzozo na Israel na njia za kumaliza migawanyiko ya ndani.

Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa na ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu hawakuwa na matumaini kwamba mikutano hiyo inaweza kutoa suluhu kwa mzozo unaoendelea kati ya Hamas na kundi la Fatah la Abbas, ambalo ni uti wa mgongo wa Mamlaka ya ndani ya Palestina.

Hii ni baada ya majaribio mengi yaliyoshindwa katika kipindi cha miaka 16 iliyopita.

Katika taarifa iliyotolewa na Hamas siku ya Jumatano, kundi hilo lilisema viongozi wake walithibitisha tena katika mkutano wa Jumanne na Abbas kwamba "upinzani ndio njia bora zaidi ya kukabiliana na makazi ya Israel."

TRT Afrika