Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitizia umuhimu wa jitihada ya haraka za kusaidia ujenzi mpya wa Syria, katika mazungumzo yake ya simu na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni.
Viongozi hao walijadiliana mgogoro wa Syria, huku Erdogan akisisitizia faida ya kuiondolea vikwazo nchi hiyo, akiitaka Italia kuwa mstari wa mbele katika mchakato huo.
Viongozi hao pia waliweka msisitizo katika kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kutatua masuala mbalimbali ya kikanda na ya kiulimwengu.
Erdogan pia aliangazia biashara iliyokomaa kati ya Uturuki na Italia, akigusia kiwango cha ujazo wa biashara kati ya nchi hizo ulifikia Dola Bilioni 32 mwaka 2024.
Kwa namna ya pekee, alionesha matumaini ya kuongeza kiwango hicho kwa kutanua wigo wa biashara na uwekezaji hasa katika sekta za ulinzi na nishati.
Nchi hizo pia zimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano katika nyanja mbalimbali na kutatua changamoto mbalimbali ulimwenguni.