Bunge la Uturuki halitatumia tena bidhaa za makampuni yanayounga mkono "uchokozi wa Israel," spika wa bunge hilo amesema.
"Katika TBMM (Bunge Kuu la Kitaifa la Uturuki), hatutatumia bidhaa zozote kutoka kwa makampuni ambayo yanaunga mkono uchokozi wa Israel," Numan Kurtulmus alisema katika hafla katika jimbo la kaskazini mwa nchi hiyo la Ordu, Jumanne.
"Hatutanunua chochote kuanzia sasa na tutatupa kile ambacho tumenunua (tayari)," Kurtulmus aliongeza.
Israel imefanya mashambulio ya anga na ardhini huko Gaza kufuatia shambulio la kuvuka mpaka la kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas tarehe 7 Oktoba.
Takriban Wapalestina 10,328 wakiwemo watoto 4,237 na wanawake 2,719 wameuawa. Idadi ya vifo vya Israeli, wakati huo huo, ni karibu 1,600, kulingana na takwimu rasmi.