Benki Kuu ya Uturuki Alhamisi imeongeza kiwango cha riba kutoka asilimia 8.5 hadi asilimia 15.
Kufuatia kuchaguliwa tena mwezi Mei, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alimleta Mehmet Simsek kama Waziri mpya wa Fedha na Hazina na mwanabenki aliyebobea Hafize Gaye Erkan kama Gavana wa Benki Kuu ya Uturuki.
"Kamati iliamua kuanza mchakato wa kubana fedha ili kuanzisha mkondo wa upunguzaji bei haraka iwezekanavyo, ili kutilia mkazo matarajio ya mfumuko wa bei, na kudhibiti tabia za bei," benki ilisema katika taarifa yake.
"Wakati mfumuko wa bei duniani umekuwa ukipungua, bado unabaki juu ya wastani wa muda mrefu. Kama matokeo, benki kuu kote ulimwenguni zinaendelea kuchukua hatua za kupunguza mfumuko wa bei.
Hatua ya benki hiyo imekuja chini ya mwezi mmoja baada ya kuteuliwa kwa waziri mpya, ambaye hapo awali alisisitiza haja ya sera ya fedha na mageuzi ya kimuundo.
"Kamati itaamua kiwango cha sera kwa njia ambayo itaunda hali ya sarafu na fedha muhimu ili kuhakikisha kupungua kwa mwelekeo wa msingi wa mfumuko wa bei na kufikia lengo la asilimia 5 la mfumuko wa bei katika muda wa kati," ilisema taarifa hiyo.
"Udhibiti wa fedha utaimarishwa zaidi kadri inavyohitajika kwa wakati na taratibu hadi uboreshaji mkubwa wa mtazamo wa mfumuko wa bei utakapopatikana."