Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki, Fahrettin Altun./Picha: AA

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki, Fahrettin Altun amesisitiza kuwa ni lazima kwa Uturuki na Uguriki kutatua matatizo yao pamoja, pasipo kuhusisha makundi mengine.

"Uturuki na Ugiriki ni lazima zitatue matatizo yao ndani ya mfumo wa maelewano na maslahi ya taifa, bila kuhitaji maelekezo," amesema Altun siku ya Jumamosi, wakati akuhutubia jukwaa la wanahabari wa Uturuki na Ugiriki, jijini Istanbul.

"Hii ndiyo sababu hasa mipango ya biashara iliyotolewa na Uturuki na Ugiriki na ina maana kubwa," aliongeza.

Mkurugenzi huyo wa Mawasiliano pia alielezea ziara ya Jumatatu ya Waziri Mkuu wa Ugiriki Kiryakos Mitsotakis, kama fursa muhimu ya kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

Akielezea kwamba Uturuki ipo tayari kuunga mkono mpango wowote ambao utaimarisha uhusiano na Ugiriki, Altun alihakikishia kwamba Ankara itadumisha msimamo huu katika siku zijazo, kwa kuzingatia "mahusiano mazuri ya ujirani na kukuza, kupanua na kubadilisha njia zetu za mazungumzo."

Akibainisha kuwa, kijiografia, Uturuki na Ugiriki zipo katika eneo lenye changamoto nyingi duniani, Altun alikumbusha kwamba nchi hizo mbili kwanza kabisa ni majirani ambao uhusiano wao unachangiwa na ukaribu wa kijiografia.

Katika hotuba yake kwa kongamano siku ya Jumamosi, Altun alisisitiza zaidi nchi za kimataifa "kwa bahati mbaya hazina ufanisi na zina upungufu wa kisiasa" katika mfumo wa sasa wa kimataifa.

"Tuko katika kipindi ambacho wanapaswa kuwa shupavu, imara na wenye ufanisi," alisema.

TRT Afrika