Magaidi wa PKK mara nyingi hujificha nje ya mpaka, kaskazini mwa Iraq, kupanga mashambulizi. / Picha: Jalada la AA

Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) "limemkata makali" gaidi mkuu wa PKK kaskazini mwa Iraqi, upande wa pili wa mpaka wa Uturuki, vyanzo vya usalama vilisema.

Gaidi huyo Celal Birdal, aliyepewa jina la Sidar Serhat, alikatwa makali katika operesheni katika eneo la Gara, duru zilisema Jumatano.

Birdal, ambaye ni mmoja wa wale wanaoitwa maafisa wa vyombo vya habari na kumbukumbu, alikuwa akifanya kazi ndani ya shirika la kigaidi wakati wa elimu yake ya uhandisi katika chuo kikuu.

Duru za usalama zinasema kuwa Celal Birdal alikuwa afisa wa vyombo vya habari na kumbukumbu wa kundi la kigaidi la PKK. Picha AA

Gaidi huyo, ambaye aliwaelekeza baadhi ya wanachama wa shirika hilo kwenda Uturuki kwa vitendo vya kigaidi, pia alikuwa mhusika wa mashambulizi mengi dhidi ya vikosi vya usalama katika mikoa ya Zap na Hakurk kaskazini mwa Iraq.

Mamlaka ya Uturuki hutumia neno "kukata makali " kumaanisha magaidi wanaohusika walijisalimisha au waliuawa au kukamatwa.

Magaidi wa PKK mara nyingi hujificha nje ya mpaka, kaskazini mwa Iraq, kupanga mashambulizi.

Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 35 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na EU - imehusika na vifo vya karibu watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake, na watoto.

TRT World