Mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson alifunga bao lake la nne ndani ya mechi ya tatu na kuipa Chelsea ushindi wa 3-2 dhidi ya Nottingham Forest  / Picha: Reuters

NICOLAS JACKSON (Chelsea)

Mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson alifunga bao lake la nne ndani ya mechi tatu na kuipa Chelsea ushindi wa 3-2 dhidi ya Nottingham Forest mwishoni mwa wiki.

Mfungaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amevumilia mwanzo mgumu wa msimu wake wa kwanza na timu ya Chelsea tangu aondoke Villarreal, lakini hivi karibuni alionyesha dalili za uzeofu wa Ligi hiyo.

Jackson alifunga bao lake la 17 msimu huu kwa kuipa timu yake ushindi dhidi ya Forest katika dakika ya 82 na kuweka timu yake katika nafasi ya kushindania kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya.

PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG (Marseille)

Mshambuliaji mkongwe wa Gabon Aubameyang alifunga bao lake la 16 katika Ligue 1 ya Ufaransa, ana mabao 29 katika mashindano yote msimu huu, ikiwa ni msimu wake wa kwanza akiichezea Marseille.

Aubameyang alifunga mara mbili kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Lorient ambayo ilifufua matumaini yao ya kufuzu Ulaya kuelekea mwishoni mwa wiki ya kampeni.

YOANE WISSA, BRYAN MBEUMO (Brentford)

Kiungo wa Kati wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Wissa alifunga kwa mara yake ya 11 msimu huu huku naye mshambuliaji wa Cameroon Mbeumo akipata bao lake la tisa ya wakati Bretford ilipoishinda Bournemouth 2-1.

ABDOULAYE DOUCOURE (Everton)

Kiungo huyo wa Mali aliipa Everton ushindi wa 1-0 dhidi ya Sheffield United, uwanjani Goodison Park.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 31 alifunga kupitia krosi iliyotoka kwa Dominic Calvert-Lewin katika dakika ya 31.

BRAHIM DIAZ (Real Madrid)

Mchezaji huyo wa Morocco amekuwa na mchango mkubwa katika ubingwa wa Real Madrid wa La Liga msimu huu na aliweza kufunga mara mbili wakati dhidi ya Granada iliyoshuka daraja, baada ya kufungwa 4-0.

YOUSSEF EN-NESYRI (Sevilla)

Mfungaji wa Morocco En-Nesyri aliiweka Sevilla mbele mara mbili dhidi ya Villarreal, ingawa timu yake ilipoteza 3-2.

Mshambuliaji huyo alifunga mabao mawili ikiwemo penalti kwenye mechi hiyo.

INAKI WILLIAMS (Athletic Bilbao)

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ghana Williams alifunga bao ambalo lilikataliwa katika mechi ya Athletic dhidi ya Osasuna, iliyomalizika 2-2. Mshambuliaji huyo aliisaidia timu yake kutoka mabao mawili nyuma hadi kumalizika sare ya 2-2.

Mchezaji wa kimataifa wa Algeria Ismael Bennacer (AC Milan) alifunga bao la kwanza la Milan kati ya mabao matano dhidi ya Cagliari kwenye ligi ya Italia, Serie A.

Aidha, mshambuliaji wa Bayer Boniface na winga Amine Adli wote wawili walifunga mabao kwenye mechi ya Bundesliga ambayo waliiadhibu Bochum 5-0.

Seerhou Guirassy wa Guinea naye aliifungia Stuttgart goli la kipekee na la ushindi wa 1-0 huko Augsburg huku timu yake ikimenyana na Bayern Munich kumaliza nafasi ya pili, katika ligi ya Bundesliga.

AFP