Beatrice Chebet baada ya ubingwa katika mashindano ya dunia ya riadha ya mbio za myika 2023 / Picha: AFP

Mbio za London, mzunguko wa mwisho wa ligi ya Wanda Diamond, kabla ya mashindano yajayo ya riadha duniani kule Budapest, yatashuhudia ushindani mkali katika kitengo cha mbio za mita 5000 za wanawake wakati mabingwa wa Olimpiki, dunia na Diamond League watatoana jasho.

Macho yote yatakuwa kwa Mkenya Beatrice Chebet, anayesifika kwa kujizolea ubingwa wa dunia wa mbio za nyika, mshindi wa mbio za mita 5000 kwenye fainali za mwaka jana ya Ligi ya Diamond, mashindano ya Afrika na michezo ya Jumuiya ya Madola.

Bingwa wa Olimpiki Sifan Hassan wa Uholanzi akifanya maandalizi yake ya Wanda Diamond League jijini London. Picha: Reuters

Beatrice Chebet atasaka ubingwa dhidi ya bingwa wa Olimpiki Sifan Hassan wa Uholanzi na bingwa wa dunia Mhabeshi Gudaf Tsegay. Mara ya mwisho aliposhindana mjini London, mnamo Aprili mwaka huu, Sifan Hassan aliondoka na ubingwa katika mbio za masafa marefu za London kwa muda wa 2:18:33.

"Mwili wangu uko katika hali nzuri kwa hivyo chochote chawezekana. Lengo langu kuu ni kuimarisha rekodi bora binafsi katika mita 5000m, na hili ni labda London, ikiwa hali itakuwa nzuri, naweza kujaribu kufanya hivyo."

Beatrice Chebet

Muethiopia Gudaf Tsegay naye sio mchache kwani amekuwa na msimu wa ajabu ikiwa ni pamoja na kuandikisha muda bora zaidi duniani wa 1500m, 3000m bila kupoteza. Pia amejinyakulia ushindi katika mbio za 1500m mjini Rabat kwa muda wa saa 3:54.03 na kushinda mbio za 10,000m katika majaribio ya Dunia ya Ethiopia kwa muda bora wa kibinafsi wa 29:29.73.

Muethiopia Gudaf Tsegay ameshinda mbio zote alizoshiriki msimu huu ikiwa pamoja na fainali za Michezo ya Dunia Picha: World Athletics

Kitengo hicho pia kitawajumuisha wanariadha chipukizi wakiwemo bingwa wa dunia kwa wanariadha chipukizi Birke Haylom, ambaye alivunja rekodi ya Afrika ya Faith Kipyegon kwa mbio za wanariadha chipukizi, Medina Eisa, Mizan Alem, na Melknat Wudu.

Mwanariadha chipukizi wa Ethiopia Birke Haylom alivunja rekodi ya Afrika ya Faith Kipyegon kwa mbio za wanariadha chipukizi. Picha AFP 

Mkimbiaji wa Afrika Kusini anayeshikilia rekodi ya dunia Wayde van Niekerk atashuka dimbani dhidi ya Mwingereza Matt Hudson-Smith anayeshikilia rekodi ya Uingereza na bingwa wa Uingereza Alex Haydock-Wilson.

Mkimbiaji wa Afrika Kusini anayeshikilia rekodi ya dunia Wayde van Niekerk. Picha AP

Kwenye mbio za mita 3000, Mkenya Beatrice Chepkoech anayeshikilia rekodi ya dunia, anaongoza orodha hiyo iliyo pia na Mwingereza Lizzie Bird, bingwa wa Uingereza Poppy Tank na Aimee Pratt.

Mwanariadha wa Ivory Coast Marie-Josee Ta Lou. Picha: AP

Mwanariadha wa Ivory Coast Marie-Josee Ta Lou naye atakimbia dhidi ya bingwa wa Marekani Sha’Carri Richardson, mshindi wa medali ya dhahabu wa dunia wa mita 200 wa Jamaica Shericka Jackson, na Waingereza Daryll Neita na Dina Asher-Smith.

Mabingwa wa mbio hizo katika vitengo vyao, watafuzu kwa Fainali ya Ligi ya Diamond ya Wanda huko Eugene ulioratibiwa kufanyika kati ya Septemba 16-17.

TRT Afrika