Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Soka Nick Mwendwa na Waziri wa Michezo Ababu Namwamba wakijadili soka. Picha: Ikulu Kenya 

Huku ombi la Afrika mashariki kuwa wenyeji wa ngarambe za Mataifa bora barani Afrika Afcon 2027, maarufu 'Pamoja' ikizidi kushika kasi, wiki hii, wawakilishi wa CAF kutoka kwa Pricewaterhouse Coopers (PwC) inayojumuisha Adam Vojtekovszk, Omar El Ghiati na Lakshmikanth Karunanithi walifanya ukaguzi wa vifaa vilivyopendekezwa kutumika kwenye zabuni hiyo kabla ya kuwasilisha kuripoti yake.

Siku chache zilizopita, maafisa hao walizuru Uganda na kukagua Uwanja wa Taifa wa Mandela unaoendelea kukarabatiwa. Rais wa FUFA Magogo Moses Hassim aliwaongoza maafisa wa Uganda katika kufanikisha ukaguzi huo.

Wawakilishi wa CAF wakagua Uwanja wa Taifa wa Mandela unaoendelea kukarabatiwa. Picha FUFA

Maafisa hao walihitimisha ziara yao Tanzania na Zanzibar walikopokewa na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Wallace Karia na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar Suleiman Mahamud.

Wakuu wa soka wa Tanzania na Zanzibar wakiwaongoza wawakilishi wa CAF Zanzibar. Picha: Shirikisho la Soka Zanzibar 

Mataifa hayo yamepewa hadi Disemba 2025 kufanikisha maandailizi na ukarabati wa miundombinu itakayotumika kwenye ngarambe hizo zenye ushindani mkali barani.

Mataifa hayo yameendeleza juhudi zao kuhakikisha ili kutimiza ndoto ya Afrika Mashariki kuandaa mashindano hayo kwani inaaminika kuwa iwapo Afrika mashariki itapokea zabuni hiyo, italeta matokeo bora yenye mchango chanya kwa ukanda mzima.

TRT Afrika