Kurejea kwa Mike Tyson kwenye ndondi kwa kutatanisha kuliishia kwa kushindwa kwa upande mmoja siku ya Ijumaa, huku mpiganaji wa tuzo ya Youtube Jake Paul akishinda kwa uamuzi wa kauli moja dhidi ya nyota huyo wa uzani wa juu huko Texas.
Tyson, 58, hakupata fursa ya kuangusha ngumi wakati wa pambano hilo la raundi nane kwenye Uwanja wa AT&T mjini Arlington, huku Paul akishinda kwa tofauti kubwa kwenye kadi zote tatu - 80-72, 79-73 na 79-73.
Paul, mwenye umri wa miaka 27, alitumia kasi na mwendo wake wa hali ya juu kumtawala Tyson aliyekuwa mzee kwa urahisi, na alimtia matatani bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu mara moja baada ya kutua kwa ngumi nyingi katika raundi ya tatu.
Hata hivyo mpiganaji huyo mdogo hakuweza kupata kipigo cha knockout alichoahidi kutoa wakati wa kupima uzito siku ya Alhamisi, ambapo Tyson alimpiga kofi usoni.
Makonde kwa mangumi
Tyson, hata hivyo, alionesha kirahisi utu uzima uliomuingia (miaka 58,) akifanikiwa kumuonjesha mpinzani wake ngumi chache tu za maana wakati wa pambano hilo.
Takwimu za mwisho zilionyesha Tyson aliunganisha ngumi 18 pekee kati ya 97 huku Paul akirusha baadhi ya ngumi 278 na kutua 78 kati ya hizo.
Sekunde za mwisho za raundi ya nane zilipokaribia, Paul aliweza hata kumudu kuinama kwa heshima ya Tyson kabla ya kengele kupigwa.