Hii ni mara ya kwanza kwa mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 27 kushiriki katika mbio za mita 150./ Photo: AFP

Mwanariadha wa Kenya Ferdinand Omanyala Jumapili aliweka rekodi mpya ya bara la africa alipotumia sekunde 14.89 katika mbio za mita 150 na kuibuka wa tatu katika Michezo ya kwanza ya Jiji la Atlanta huko Georgia, Marekani.

Amevunja rekodi ya Afrika ya sekunde 14.99, ambayo iliwekwa na mwanariadha wa Namibia Frankie Fredericks mwaka 1993.

Mwanariadha wa Marekani Lyles Noah alishika nafasi ya kwanza katika mbio za mita 150 katika michezo ya Atlanta baada ya kutumia sekunde 14.56.

Omanya amevunja rekodi ya Afrika ya sekunde 14.99, ambayo iliwekwa na mwanariadha wa Namibia mwaka 1993. Picha/Getty Images

Mshiriki wa Noah, Erriyon Knighton, alikamilisha mbio kwa sekunde 14.85 kuchukua nafasi ya pili. Omanyala alikuwa amejifunga kwa mtindo wa kusisimua lakini alishindwa kuelekea mwisho wa mbio.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 27 kushiriki katika mbio za mita 150, mbali na mbio zake za mita 100. Mshika rekodi huyo wa Kiafrika sasa anarejea Kenya kwa ajili ya tamasha la Kip Keino Classic linalotarajiwa kufanyika Mei 13.

Mnamo Septemba 18, 2022, aliweka rekodi ya Afrika ya mita 100 baada ya kutumia sekunde 9.77 jijini Nairobi.

Mnamo 2022, alishinda ubingwa wake wa kwanza wa kimataifa, na ushindi katika mbio za mita 100 kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola ya Birmingham na Mashindano ya Afrika katika Riadha.

Mnamo Septemba 18, 2022, aliweka rekodi ya Afrika ya mita 100 baada ya kutumia sekunde 9.77 jijini Nairobi.

TRT Afrika