Edin Dzeko
Nahodha wa Bosnia na Mshambulizi wa zamani wa Manchester City na Inter Milan, Edin Dzeko alitia saini mkataba wa miaka miwili na Fenerbahce kwa uhamisho wa bure.
Alex Oxlade-Chamberlain
Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain, amewasili Besiktas. Nyota huyo aliyeshuhudia msururu wa muda mrefu zaidi bila kushindwa katika historia ya Liverpool (mechi 39) hatimaye amechagua Uturuki licha ya kupokea ofa ya Saudia.
Fred
Kiungo wa kati wa Brazil, Fred naye ameefululiza kwenda Fenerbahce na kuiaga Manchester United. Kiungo huyo wa kati amehamia Fenerbahce kuweza kuingia uwanjani kucheza zaidi katika kikosi cha kwanza ingawa alikuwa amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake United.
Wilfried Zaha
Winga mwenye uzoefu, Wilfried Zaha naye ameondoka Crystal Palace hadi wababe wa Uturuki, Galatasaray baada ya kuhudumu katika klabu yake ya Crystal Palace kwa muda mrefu.
Eric Bailly
Eric Bailly, Beki wa zamani wa Manchester United amejiunga na Besiktas na kuondoka Old Trafford huku akisaini mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo ya Uturuki.
Tanguy Ndombele
Kiungo matata Tanguy Ndombele amewasili Galatasaray baada ya kuhama Tottenham Hotspur. Mchezaji huyo wa zamani wa Lyon na Napoli, alisajiliwa kwa njia ya mkopo.
Davinson Sanchez
Difenda Davinson Sanchez wa Tottenham Hotspur naye ameguria Galatasaray na kusaini mkataba wa miaka minne kupiga ligi ya Uturuki
Hakim Ziyech
Hakim Ziyech wa Chelsea naye amejiunga na Galatasaray baada ya kuzisaidia Chelsea na Morocco msimu uliopita. Licha ya uhamisho wake wa kwenda PSG na Al-Hilal kugonga mwamba, mchezaji huyo amehamia Uturuki na kupokewa kwa shangwe.
Daniel Amartey
Beki wa timu ya taifa ya Ghana, Daniel Amartey naye amejiunga na Besiktas kwa kuondoka Leicester City baada ya misimu minane na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Arthur Masuaku
Arthur Masuaku ameihama West Ham United kwenda Besiktas kwa njia ya mkopo. Beki huyo wa kushoto aliyecheza mechi 105 za Premier League atasalia Uturuki baada ya timu hizo kufikia makubaliano.