Patrick Kluivert anamrithi Vincenzo Montella kwenye benchi ya Adana Demirspor. Picha: Reuters

Klabu ya Uturuki Adana Demirspor imemteua mchezaji wa zamani wa Uholanzi na FC Barcelona Patrick Kluivert kama kocha mkuu siku ya Jumamosi.

"Klabu yetu imetia saini mkataba wa miaka miwili na Patrick Kluivert kwa wadhifa wa kocha mkuu. Karibu Patrick Kluivert," klabu hiyo ya kusini mwa Uturuki iliandika kwenye Twitter.

Kluivert aliletwa kwa nafasi iliyoachwa wazi kwani Muitaliano Vincenzo Montella aliondoka katika klabu hio ya Uturuki ya Süper Lig mwezi Juni.

Mmoja wa wachezaji maarufu wa kizazi chake, Kluivert, 47, alichezea klabu ya Uholanzi Ajax kabla ya kujiunga na AC Milan, uzoefu wake wa kwanza nje ya nchi.

Patrick Kluivert anamrithi Vincenzo Montella kwenye benchi ya Adana Demirspor. Picha: AFP

Aliajiriwa na FC Barcelona mnamo 1998, ambapo alijitofautisha na uchezaji wake.

Kluivert alishinda 1995 UEFA Champions League akiwa na Ajax, akifunga bao la ushindi kwenye fainali dhidi ya Milan, ambayo iliisha 1-0 huko Vienna.

Alishinda mataji ya Uholanzi akiwa na Ajax na PSV Eindhoven, pamoja na La Liga ya Uhispania akiwa na Barcelona.

Kluivert amefunga mabao 40 katika mechi 79 alizoichezea Uholanzi.

Kabla ya kuanza kazi yake mpya Adana Demirspor, Kluivert alikuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ya Curaçao.

Curacao, iliyoko Karibiani, ni jimbo huru lililounganishwa na Uholanzi.

AA