Rais wa Yanga Hersi Ally Said atawasimamia viongozi wenzake kwenye soka barani Afrika. Picha: CAF

Rais wa mabingwa wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Hersi Ally, ndiye ametwikwa jukumu la kuongoza, uongozi mpya wa chama kipya cha vilabu vya soka barani Afrika (ACA) uliochaguliwa mjini Cairo, Misri kwenye uzinduzi wa ACA.

Rais wa CAF Patrice Motsepe aliongoza uzinduzi huo wa muungano wa vilabu vya soka Afrika uliohudhuriwa na watendaji wakuu na wenyeviti wa vilabu vya Soka Afrika Cairo, Misri.

Hersi atasaidiwa na manaibu wawili: Jessica Motaung kutoka timu ya Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) na Paul Bassey wa Akwa United ya Nigeria kuongoza vilabu katika mataifa 54 vya wanachama wa CAF.

Muungano huo wa Klabu za Afrika unalenga kuleta pamoja wadau wote wa soka barani Afrika, ili kukuza ushirikiano, uvumbuzi, na ubora ndani ya sekta ya soka kwa klabu Afrika.

Hersi atahusika kuongoza juhudi za kulinda na kukuza maslahi ya Klabu za Soka barani.

Kuhakikisha kwamba Klabu za soka za Afrika zina faida kibiashara, na ushindani wa kimataifa na faida.

Kujenga ushirikiano na wadhamini, sekta binafsi na serikali ili kufanikisha ujenzi wa viwanja vinavyotimiza viwango vya CAF na FIFA na miundombinu na vifaa vingine vya mpira wa miguu katika kila moja ya vyama 54 vya wanachama wa CAF.

TRT Afrika