Kiungo wa Klabu ya Juventus na Timu ya Taifa ya Ufaransa Paul Pogba / Picha: AFP

Kiungo wa Klabu ya Juventus na Timu ya Taifa ya Ufaransa Paul Pogba amepigwa marufuku kucheza soka kwa miaka minne na Mahakama ya kupambana na dawa za kulevya nchini Italia.

Pogba alipigwa marufuku baada ya kupimwa na kupatikana na testosterone Agosti mwaka jana, Klabu yake ya Juventus ilisema Alhamisi.

Hata hivyo, wawakilishi wa Pogba wamesema kuwa dawa hiyo ya testosterone ilitokana na nyongeza ya kiungo kwenye chakula iliyowekwa na daktari aliyemshauri, Marekani.

Pogba anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo nchini Uswisi.

Pogba alirejea Juventus kutoka Manchester United mnamo 2022 lakini alikabiliwa na majeraha, akicheza mechi 6 pekee Serie A, Juventus msimu uliopita na mbili msimu huu.

Kati ya 2012-16, Pogba alicheza mechi 178 kwa Juventus.

Pogba aliisaidia Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia 2018, akifunga katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Croatia kwenye fainali.

Kati ya 2012-16, Pogba alicheza mechi 178 kwa Juventus.

TRT Afrika na mashirika ya habari