Erling  Haaland wa Manchester City / Picha: Reuters

Manchester City wametoa sare yao ya pili kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, wakati huu mbele ya Newcastle United waliokuwa nyumbani St James' Park, siku ya Jumamosi.

Manchester City ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani wao katika dakika ya 35, kupitia kwa beki wa kulia Josko Gvardiol, aliyepokea pasi kutoka kwa Jack Grealish katika mchezo huo ulioshuhudia kadi nane za njano zikitolewa na mwamuzi wa mchezo huo.

Newcastle walisawazisha katika dakika ya 58 ya mchezo kupitia mkwaju wa penati, baada ya kipa Ederson, kumkwatua Anthony Gordon aliyekuwa anaelekea kufunga.

Kwa sasa, City imefikisha alama 14 baada ya michezo sita, huku ikiwasubiria Liverpool, Aston Villa na Arsenal kushuka dimbani, wakati Newcastle United ina alama 11, ikishika nafasi ya tano.

TRT Afrika