Nasra Ali ambaye ameiwakilisha Somalia mashindano ya kimataifa ya riadha. Picha: SONNA

Wizara ya michezo ya Somalia, imesema kuwa mkimbiaji aliyeonekana kwenye mashindano ya michezo ya kimataifa ya vyuo vikuu vya Dunia ya FISU, ni mwanariadha bandia.

Nasro Ali Abukar, aligeuka kuwa kicheko cha taifa huku raia wa Somalia wakionyesha ghadhabu kwa matokeo yake alipomaliza wa misho katika mbio hizo na kuweka rekodi ya mkibmiaji aliyemaliza kwa muda mbaya zaidi kwenye historia ya mashindano hayo.

Nasra Abukar Ali, 20, alimaliza mbio za mita 100 kwa muda wa sekunde 21, huku watumiaji wa mtandao wakimtaja kuwa "mwanariadha mbaya zaidi" katika makala ya 31 ya michezo ya vyuo Kikuu Duniani cha Majira ya joto huko Chengdu, China.

Waziri wa michezo Somalia Mohamed Bare./ Picha: Wizara ya Michezo Somalia

Waziri wa Michezo Mohamed Bare, amesema kupitia taarifa kuwa mwanaridha huyo aliteuliwa kimagendo kupitia taratibu zisizoeleweka na kuleta aibu kwa taifa kwenye jukwaa la kimataifa.

Kufuatia sakata hiyo, Waziri wa Michezo wa Somalia Mohamed Bare Mohamud amemuachisha kazi mkuu wa shirikisho la riadha la Somalia, Khadija Adan Dahir, kwa tuhuma za "kutumia vibaya mamlaka yake na kumteua mwanariadha asiye na taaluma kuliwakilisha taifa.

Rais wa shirikisho la riadha la Somalia, Khadija Adan Dahir. Picha: SONNA. 

Aidha, waziri huyo amekana kuhusika kwa wizara yake au kufuatwa kwa taratibu mwafaka katika uteuzi wa wanariadha huyo kushiriki kwenye michezo.

Awali, Waziri huyo wa Michezo wa Somalia aliomba msamaha kufuatia sakata hiyo.

Tunaomba msamaha kwa jamii nzima ya Wasomali. Kwa kweli, yaliyotokea ni aibu kwa bendera ya nchi na jamii ya Wasomali. Wizara ya michezo haifahamu jinsi alivyochaguliwa kuliwakilisha taifa.

Waziri wa Michezo Mohamed Bare

Somalia imesema itamfungulia mashtaka Khadija Adan Dahir kwa kukiuka taratibu za kuwateua wawakilishi wa nchi kwenye mashindano ya viwango vya juu na kushusha hadhi ya nchi hiyo.

TRT Afrika