Ronaldo alikamilisha usajili wake klabu ya Al Nassr. Picha: Al-Nassr      

Al-Nassr imenyanyua mataji tisa ya ligi kuu, sita ya Kombe la Mfalme, matatu ya kombe la Crown Prince, matatu ya Kombe la Shirikisho na mawili ya Saudi Super Cup. Klabu hiyo imewasaini Ronaldo, Sadio Mane na Marcelo Brozovic

  • Cristiano Ronaldo, Al-Nassr: £173m kwa mwaka, au £3.4m kwa wiki
  • Sadio Mane, Al-Nassr: £34m kwa mwaka, au £650,000 kwa wiki
  • Marcelo Brozovic, Al Nassr: £35m kwa mwaka, au £403,000 kwa wiki

Al-Ittihad ni timu ya pili yenye ufanisi mkubwa nchini Saudi Arabia, kwani imeshinda mataji tisa ya ligi, matano ya King's cup, nane ya Crown Prince Cup, matatu ya Saudi Federation Cup na moja ya Saudi Super Cup.

  • Karim Benzema £172m kwa mwaka, au £3.3m kwa wiki
  • N'golo Kante Al £86.2m kwa mwaka, au £1.6m kwa wiki

Karim Benzema ameshinda Ballon d'Or - tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka 2022. Picha: Al-Ittihad

Klabu ya Al Ahli SFC, kama tu Al Ittihad, ni timu kutoka mji wa bandari wa Saudi wa Jeddah, na imefanikiwa kuwanasa Roberto Firmino, Edouard Mendy na Riyad Mahrez waliohama kutoka ligi kuu ya soka ya Uingereza. Al-Hilal imewasajili wachezaji watatu kati ya wanne ghali zaidi katika historia ya Saudi Pro League.

Riyad Mahrez mazoezini katika klabu yake mpya ya Al AHLI ya Saudi. Picha: Al Ahli.

  • Riyad Mahrez: £25.6m kwa mwaka, au £750,000 kwa wiki
  • Roberto Firmino: £17m kwa mwaka, au £326,000 kwa wiki
  • Edouard Mendy: £9.4m kwa mwaka, au £230,000 kwa wiki

Klabu ya Al-Hilal ndio klabu ilitwaa mataji mengi zaidi katika soka la Saudia ikiwa imeshinda ligi mara 18. Aidha, Al-Hilal imejinyakulia mataji manne ya Ligi ya Mabingwa ya bara Asia, yaani AFC

Kalidou Koulibaly amehama blues wa uingereza Chelsea na kutua blues wa Saudi Al-Hilal. Picha: Al Hilal. 

  • Kalidou Koulibaly Al-Hilal £30m kwa mwaka, au £300,000 kwa wiki

Al Ettifaq inayoongozwa na Steven Gerrard, imebeba ligi hiyo mara mbili. Timu hiyo imemnasa Jordan Henderson kutoka klabu ya Liverpool ya Uingereza.

  • Jordan Henderson Al-Ettifaq: £18.2m kwa mwaka, au £692,000 kwa wiki

TRT Afrika