Orodha fupi ya wanasoka bora wa kiume kuwania tuzo za CAF 2023. Picha: CAF

Mshindi anatarajiwa kutangazwa rasmi kwenye hafla itakayofanyika Jumatatu, tarehe 11 Desemba 2023, katika ukumbi wa Palais des Congrès, Movenpick, mjini Marrakech, nchini Morocco.

Wanasoka waliosakata soka kikosi kimoja katika klabu ya Liverpool, Sadio Mane na Mohamed Salah, kwa mara nyingine watatoana jasho baada ya kujumuishwa kwenye orodha ya 10 bora iliyozinduliwa na CAF.

Aidha, timu ya taifa ya Morocco ndio yenye wachezaji wengi kwenye orodha hiyo, kwani ina wachezaji wanne kufuatia uhodari wao wa kuweka historia kombe la dunia 2022 ambapo ilifika nusu fainali.

Wachezaji hao wa Morocco ni pamoja na Achraf Hakimi wa Paris Saint-Germain ya Ufaransa, Sofyan Amrabat anayesakata na klabu ya Manchester United, Yassine Bounou anayechezea Al Hilal nchini Saudi Arabia, na Youssef En-Nesyri wa klabu ya Uhispania ya Sevilla.

Wachezaji 10 waliotangazwa na CAF kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika 2023.

  • Riyad Mahrez (Algeria, Al Ahli)
  • Andre-Frank Zambo Anguissa (Cameroon, SSC Napoli)
  • Vincent Aboubacar (Cameroon, Besiktas)
  • Mohamed Salah (Misri, Liverpool)
  • Achraf Hakimi (Morocco, Paris Saint-Germain)
  • Sofyan Amrabat (Morocco, Manchester United)
  • Yassine Bounou (Morocco, Al Hilal)
  • Youssef En-Nesyri (Morocco, Sevilla)
  • Victor Osimhen (Nigeria, SSC Napoli)
  • Sadio Mane (Senegal, Al Nassr)

Jopo la wapiga kura linalojumuisha kamati ya Ufundi ya shirikisho la soka Afrika CAF, wataalamu wa vyombo vya habari, Makocha wakuu na wakuu wa mashirikisho wanachama na vilabu vinavyoshiriki katika hatua za makundi ya mashindano ya klabu barani, watapiga kura kuamua mshindi.

Vitengo vingine vitakavyotouzwa ni pamoja na kipa bora wa mwaka, chipukizi bora wa mwaka (U21), Kocha bora wa mwaka, timu bora ya taifa ya mwaka na klabu bora ya mwaka.

TRT Afrika na mashirika ya habari