Ahmed Refaat alikuwa akichezea klabu ya Modern Sport ya Misri/ Picha : Reuters 

Mchezaji wa kimataifa wa Misri Ahmed Refaat amefariki akiwa na umri wa miaka 31, klabu yake ya Modern Sport ilisema Jumamosi, kufuatia mshtuko wa moyo wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Misri mwezi Machi.

Refaat aliwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi mnamo Machi 11 baada ya kuzimia katika dakika ya 88 ya mechi ya ligi ya Modern Future dhidi ya Al-Ittihad Alexandria.

Mshambulizi huyo ambaye alikuwa amewekewa kifaa cha kudhibiti moyo, aliruhusiwa kwenda nyumbani mwezi mmoja baadaye na kuendelea kupata matibabu.

Shirikisho la Soka Afrika (“CAF”) lilichapisha habari ya tanzia katika mtandao wake na kuitakia familia ya Refaat uvumilivu.

Nyota wa Misri anayechezea klabu ya Liverpool Mohammad Salah, alituma rambirambi katika mtandao wa X akielezea kuhuzunishwa kwake na kuwapa subira familia yake na wote wapendwa wake wote wakati huu mgumu.

Wengi waliandika katika mtandao wa kijamii, ''Sote tumetoka kwake na kwake tutareje..''

TRT Afrika