Bara Afrika halijawahi kuandaa Michezo ya Olimpiki. Mara ya mwisho Cairo ilitoa ombi halikufanikiwa kwa Olimpiki ya 2008./ Picha : Reuters 

Misri itawasilisha ombi la kuandaa Olimpiki ya Majira ya joto ya 2036 na 2040, huku uboreshaji wa miundombinu na vifaa vya michezo nchini humo ni muhimu kwa ajili ya ombi la Afrika lenye mafanikio, alisema mkuu wa chama cha kamati za kitaifa za Olimpiki barani Afrika (ANOCA) Jumapili.

Bara Afrika halijawahi kuandaa Michezo ya Olimpiki. Mara ya mwisho Cairo ilitoa ombi halikufanikiwa kwa Olimpiki ya 2008.

Nchi yenye watu wengi zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu, Misri imetumia mabilioni ya dola kujenga vifaa, viwanja vya michezo na miundo mbinu ya michezo katika miaka ya hivi karibuni kama sehemu ya mipango yake ya kuifanya nchi hiyo kuwa ya kisasa.

Uwanja wa mji mpya wa Kimataifa wa Olimpiki wa Misri katika mji mkuu mpya wa utawala ambao nchi hiyo imekuwa ikijenga mashariki mwa Cairo tangu 2015 unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua watu 93,900 na vifaa vingine 21 vya michezo.

"Misri itajinadi kwa 2036 na 2040," Mustapha Berraf, mkuu wa ANOCA aliambia mkutano wa waandishi wa habari siku ya kufunga sherehe za Olimpiki za Paris.

Msimamizi huyo wa michezo wa asili ya Algeria alisema ombi lingine la Kiafrika linaweza kutimizwa na Cape Town ya Afrika Kusini ikifikiria kugombea Olimpiki. Hata hivyo, hakusema itaomba kwa Michezo gani.

"Afrika ina nafasi ya kuandaa Michezo hiyo. Kuna uwezekano mkubwa kuandaa Michezo hiyo mwaka wa 2040," alisema Berraf, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.

"Kuna haja ya kuangalia masuala ya miundombinu kama vile barabara, viwanja vya ndege. Misri ina uwezo muhimu wa miundombinu."

Los Angeles watakuwa wenyeji wa Michezo ya Majira ya joto ya 2028 huku Brisbane ya Australia ikijiandaa kuandaa Olimpiki ya 2032.

Tayari kuna nchi na miji kadhaa inayotaka zabuni ya kuandaa Olimpiki ya 2036 ikijumuisha Indonesia, India, Uturuki, Qatar na Saudi Arabia.

Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach amesema nia ya kuandaa Olimpiki ya 2036 hadi sasa imevutia miji zaidi ya kumi.

TRT Afrika
Reuters