Mchezaji wa Dinamo Bucharest Edgar Le ameshtakiwa kwa kuwakilishwa na ndugu yake pacha kwenye mechi.
Inashukiwa kuwa ndugu pacha, Edelino aliweza kucheza angalau mechi 5 na ikiwa madai hayo yatathibitishwa baada ya vipimo vya DNA, huenda klabu ya Dinamo Bucharest itashushwa kutoka ligi na kulishwa adhabu ya kupokonywa alama.
Kwa upande mwengine, kiungo Edelino, ambaye ni mwanasoka kama Edgar, ametumikia tu katika timu za daraja za chini za Ureno kwenye taaluma yake.
Taarifa za vyombo vya habari vya Kiromania zilidai kuwa, Edgar, ambaye alijiunga na Dinamo Bucharest msimu huu, alianza kumtuma ndugu yake pacha Edelino kwenye timu badala ya kucheza mwenyewe.
Nyota huyo ni mchezaji wa timu ya taifa ya Guinea-Bissau, na wakati mmoja aliwakilisha klabu za Feyenoord, Lille, Nantes, na timu za Uturuki za Trabzonspor na Başakşehir, baada ya kuaza safari na timu ya chipukizi ya Barcelona.
Edgar, mwenye umri wa miaka 30, ametokea mara chache uwanjani katika wiki za hivi karibuni kutokana na fomu duni licha ya kuwa mchezaji wa klabu anayelipwa zaidi.
Kwa upande wake, klabu ya Dinamo Bucharest imepinga madai hayo.
"Kusema kwamba Dinamo Bucharest ina shaka kwamba haikuhamisha Edgar Lé, na kaka yake pacha, Edelino Miguel Ié, ni uwongo, kashfa, na shambulio sawa na saratani dhidi ya kilabu," Dinamo imesema.