Nyota wa AFCON Cote D'ivoire 2023 wakiwa na nyuso za furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao. /Picha: CAF

Pazia la AFCON limefungwa kwa Cote D' Ivoire kunyakuwa taji hilo, tukio lilishuhudia kutunukiwa kwa wachezaji bora wa michuano hiyobaada ya mapazia kufungwa rasmi kwenye mashindano ya Afcon, shirikisho la soka barani Afrika CAF liliwatunuku wanasoka bora wa mashindano hayo.

Nahodha wa Nigeria, William Troost-Ekong aliondoka na tuzo ya Mchezaji bora wa AFCON.

Mfumania nyavu kutoka Equatorial Guinea, Emilio Nsue Lopez alizadiwa kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika.

Kwa upande wake, mlinda mlango wa Bafana Bafana, Ronwen Williams alichaguliwa kama kipa bora wa michuano hiyo, ilitolewa na Ecobank kwa ushujaa wake ulioiwezesha Afrika kusini kushika nafasi ya tatu katika michuano hiyo na kupata medali ya shaba. Williams atakumbukwa kwa uhodari wake wa kupangua mikwaju minne dhidi ya Cape Verde, na mingine miwili walipokutana na DRC.

Bafana Bafana, pia walipata tuzo ya 'Fair Play', kwa kuonesha mchezo wa kiungwana kwenye mashindano hayo.

Aidha, nyota wa pasi mbili za Cote D'ivoire kwenye fainali hiyo, Simon Adingra (22) alitunukiwa tuzo ya chipukizi bora wa AFCON kwa mwaka 2023.

Adingra pia alitia kapuni tuzo moja nyingine baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa katika mechi ya fainali, wakati Kocha Emerse Faé wa Cote D'ivoire alitwaa tuzo ya kocha bora wa michuano hiyo.

TRT Afrika