Gervais Hakizimana, aliyehusika kwenye ajali ya barabarani iliyosababisha vifo vya wawili hao, amezikwa nchini Rwanda.
Mwanariadha maarufu kutoka Kenya Kelvin Kiptum na kocha wake kutoka Rwanda Hakizimana walikuwa wakilenga kushiriki mbio za Rotterdam Marathon za mwezi Aprili Uholanzi, kabla ya kukutana na vifo vyao.
Gervais Hakizimana alihamia Kenya mnamo 2006, kutoka Rwanda alipokuwa akikaribia mwishoni mwa ujana wake.
Hakizimana na Kelvin Kiptum walikutana 2013, kipindi Kiptum bado alikuwa mwanariadha chipukizi.
Waziri wa Michezo wa Kenya Ababu Namwamba, aliiwakilisha serikali ya nchi hiyo, na kutaja kifo cha wawili hao kuwa pigo kwa Afrika Mashariki na Ulimwengu kwa ujumla.
Kiptum alikuwa akilenga kuweka historia kwa kuwa mwanariadha wa kwanza rasmi wa mbio za marathon kumaliza mbio kwa chini ya saa mbili katika historia.