Angola inaatarajiwa kutumia bahati ya kuchezea nyumbani kujinyakulia ubingwa wake wa kwanza wa shindano la AfroCan, linaloanza Julai 8.
Hii ni mara ya pili kwa nchi hiyo kushiriki shindano hili ambapo walimaliza watatu katika duru ya kwanza kuchezwa nchini Mali mwaka 2019.
Angola hata hivyo ina historia ya kufanya vyema wakiwa nyumbani ambapo kwa zaidi ya miaka 30 wameshindwa mara moja pekee walipocharazwa na Cote di’Voire katika ngome yao wakati wa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia kwa timu za Afrika, Novemba 2021.
Kwa upande wake Kenya wanaingia jukwaani kifua juu kama moto wa kuotea mbali, kwani duru ya kwanza wlaifika Fainali na kufungwa na Jamhuri ya demokrasia ya Congo, ambao waliyakua kombe.
Hii ni fursa nzuri kwa Kenya kuonesha ushupavu wao katika mpira wa vikapu barani Afrika wanapopambana na Cote di’Voire Jumamosi katika uwanja wa Kilamba nje yamji mkuu Luanda.
Kocha wa Kenya Cliff Owuor aliambia shirika la habari la Capital FM kuwa vijana wake wameiva kutwa aubingwa mwaka huu.
‘’Hakika kuna shinikizo fulani lakini tulipaswa kuikumbatia ikiwa tunataka kushinda. Tunajua tuna watu wanaotu shabikia nyuma yetu na kutuunga mkono na tunataka kuiwakilisha nchi vyema. Tutajaribu kupanda juu ya shinikizo hilo na kufanya,’’ alisema Owuor.
Morans wa Kenya wameorodheshwa katika kundi A pamoja na Cote di’Voire na Gabon.
Utaratibu wa mechi
Huku timu nane zikiwa zinarudi tena kwa mara ya pili tangu kuzinduliwa kwa michezo huu mjini Bamako Mali mwaka 2019, kunao wanaoingia mara ya kwanza kama vile - Cameroon, Gabon, Msumbiji na Rwanda.
Timu zimegawanywa katika vikundi vinne vya timu tatu kila moja. Timu zitakazomaliza katika nafasi za kwanza za Kundi A,B,C na D zitafuzu moja kwa moja hadi Robo Fainali.
Timu zitakazomaliza katika nafasi za pili na tatu za kila kundi, zitapata fursa nyingine ya kujitafutia nafasi katika robo fainali kwa kucheza Raundi ya Mchujo, ambapo timu zitakazopoteza zitatolewa
Timu nne zilizofuzu nusu fainali zitafuzu moja kwa moja kwa FIBA AfroCan 2027 huku timu zilizoshindwa katika Robo Fainali zitachuana kwa Nafasi ya tano hadi nane katika raundi ya uainishaji.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ndio mabingwa watetezi.