September 11, 2001. Miaka 22 kabla, nikiwa nimerudi Marekani kutoka moja ya nchi za Afrika Magharibi ambayo raia wengi wa Marekani, pengine hawajawahi kuisikia, Niger.
Hivi sasa, bila shaka, tunaweza kusema Niger imekuwa maarufu, au sio maarufu, inategemea na mtizamo wa mtu – hii ni kutokana na mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibuni ambayo yalimuondoa madarakani kiongozi aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, na kuweka utawala wa Baraza la Usalama wa Taifa –kwa maana nyengine junta.
Moja ya sababu kuu iliyotolewa ya kupindua serikali mjini Niamey ilikuwa ni kushindwa kwa mkakati wa rais Bazoum wa kupambana na ugaidi ndani na pembezoni mwa mipaka ya nchi yake.
Kwa sadfa, nilikuwa nimerudi nchini Niger wakati wa mapinduzi kwa kazi maalumu na Tume ya Taifa ya Mipaka.
Katika bara ambalo, limeshuhudia zaidi ya mapinduzi ya kijeshi mia moja tangu Afrika kujipatia uhuru kutoka kwa wakoloni, zaidi ya miongo sita iliyopita, mapinduzi matano yaliyofanyika nchini Niger, hayakuwa na athari kubwa.
Kwamba, ugaidi, umetumika kama sababu kuu ya mapinduzi, ni jambo jipya.
Ni kwa kiasi gani, dunia, na hasa Afrika, imebadilika tangu Al Qaeda walipoyapindua majengo mawili ya biashara ya World Trade Center, na kutangaza vita na Marekani.
Haikuchukua muda kwa Marekani kuwasambaratisha Osama Bin Laden na wafuasi wake katika maficho yao huko Afghanistan, ikiibua swali muhimu: wapi pengine magaidi hao wataibuka tena? Wapi watakimbia, wapi watapata hifadhi, na wapi watajipanga upya?
Utafutaji wa Uranium
Wana mikakati wa kijeshi wa Marekani walitarajia kwamba itakuwa chuki dhidi ya waislamu duniani kutokana na mapaka isiyodhibitiwa, uwezo mdogo wa serikali, na ufukari ulioenea. Sahel. Hivyo ikaanzishwa, mapema mwaka 2002, mpango wa Pan-Sahel, PSI wenye lengo la kusaidia nchi kadhaa kufuatilia harakati za watu.
Mwanzoni, PSI iliweka, chini ya jicho la Marekani, nchi kama Niger, Chad, Mali and Mauritania katika jitahada za kutabiri kuibuka kwa kile kilichoitwa, ‘’Ugaidi wa Kiislamu’’ katika eneo hilo la Afrika Magharibi.
Ni mazingira hayo yaliyoifanya Niger kuibuka katika macho ya Marekani, ilitangazwa na aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo George W. Bush mwaka 2003 kama njia ya kuwawinda Al Qaeda – au uranium kwa Saddam Hussein kwa kisingizio cha mpango wa kuharibu silaha za maangamizi.
Lakini haijalishi, hasara ilikuwa ishafanyika: Sahel itafahamika kama kiunganisha muhimu katika mtandao wa ugaidi duniani, ambao ulipelekea kuibuka kwa kilichoitwa kikundi kijulikanacho kama Daesh, na matawi yake kadhaa, kuanzia nchini Iraq na Syria (ISIL) mpaka eneo la Maghreb (Ansar al Sharia) mpaka Afrika Magharibi (ISWA).
Hatimae, PSI ikabadilika na kuwa Trans-Sahara Counter-Terrorism Partnership (TSCTP), ambayo hii leo, inahusishwa nchi 12 za Sahel na Maghreb.
Iwapo malengo ya PSI na TSCTP yalikuwa na uhalisia au yalikuwa na lengo la kutimiza matakwa binafsi, itabakia kuwa mjadala miongoni mwa wabobezi na wataalamu wa kijeshi katika eneo hilo.
Lakini uhalisia ni kwamba, nzige wa ugaidi amehama kutoka mashariki ya kati mpaka Afrika Magharibi na zaidi
Na iwapo itahusishwa au la, kudhoofika kwa uwezo wa ISIS na Al Qaeda nchini Iraq na Syria, kumekuja pamoja na kudhoofika kwa ushawishi wa Ufaransa katika eneo la Afrika Magharibi.
Upweke wa Marekani
Chuki dhidi ya Ufaransa imekuwa ni sera ya wanaotaka kuchukua madaraka kwa nguvu nchini Burkina Faso, Guinea na Mali – hivi sasa wakifuatiwa na Niger katika utawala wa kijeshi na chuki dhidi ya Ufaransa.
Marekani haikufurahia kuibadilisha Ufaransa kama polisi mkubwa dhidi ya ugaidi, katika uwezeshaji wa vifaa na ushauri.
Lakini Ufaransa ikiwa inaweka vizuri majeshi yake nchini Mali na Niger, na sasa hivi wanashinikizo la kuwaondoa kutoka Niger, Marekani inaweza kubakia pekee kubeba mzigo.
Miaka ishirini na mbili iliyopita, “matumizi ya ndege” ambazo zilianguliwa katika milima ya Asia ya kati yalifanyika.
Serikali husika, Ufaransa, Marekani na Afrika, wana jukumu la kuepusha uhalifu kama huo kutokea sehemu nyingine.
Wakati hayo yakijiri, mapambano dhidi ya ugaidi, hawezi kamwe kuwa kisingizio cha kupindua serikali.
Mwandishi, William F.S. Miles ni profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Northeastern. Aliyekuwa Mjitolea wa Peace Corps (1977-1979) nchini Niger na Msomi wa Fulbright huko (1983-4, 1986), ndiye mwandishi wa Hausaland Iliyogawanywa: Ukoloni na Uhuru nchini Nigeria na Niger na Tatizo Langu la Farasi wa Kiafrika.
Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi si lazima yaakisi maoni, maoni na sera za uhariri za TRT Afrika.